Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mgogoro wa ardhi: Rais Magufuli ampa siku 7 Waziri Lukuvi
Habari za Siasa

Mgogoro wa ardhi: Rais Magufuli ampa siku 7 Waziri Lukuvi

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Magufuli, amempa siku saba William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, amkabidhi  hati ya shamba lenye ukubwa wa hekta 5,000, linalomilikiwa raia wa kigeni wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilosa … (endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020, baada ya kupokea malalamiko ya mgogoro wa ardhi, kutoka kwa wananchi wa Kibamba, wilayani Kilosa.

Kiongozi huyo wa Tanzania, amemuagiza Waziri Lukuvi aliyekuwepo kwenye msafara wake kumkabidhi hati ya shamba hilo, ili aligawe upya, kisha  sehemu yake wapewe wananchi wa Kibamba, kwa ajili ya kumaliza changamoto ya mgogoro wa ardhi.

“Kibamba inaonekana kuna matatizo makubwa na sijawahi kuona mahali kuna matatizo ya ardhi kama hapa, ninawaomba sana, ndugu zangu waziri wangu yuko hapa na nina muamini sana. nishaelekeza ndani ya wiki moja watakuja hapa,” amesema Rais Magufuli

“Kuanzia leo waanze kushughulikia hapa, zile hati au mashamba yanayotakiwa kufutwa atayaleta waziri, nataka kabla ya Jumamosi yafike kwangu kwa mkono na nitasaiini saa hiyo hiyo ili yatekelezwe,” amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa na wananchi waliojitokeza kumsikiliza

Rais Magufuli amesema katika uongozi wake, atahakikisha analinda maslahi ya wananchi wanyonge, pamoja na kuwadhibiti wenye nguvu ambao wamekuwa wanadhurumu haki za wanyonge.

Rais John Magufuli, akiwahutubia wananchi wa Kilosa

“Mnakodishiwa (mashamba) sababu hati ni za wakubwa, nataka nilale nao hao wakubwa, nimesema siku saba waziri pamoja na mkuu wa mkoa ataleta hati, yale mashamba yakufuta, sababu kwa mujibu wa sheria ardhi iko chini ya rais, na mimi nitaenda na watu wanyonge,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Kibamba, kutumia vyema mashamba watakayopewa.

“Naweza futa nusu au kutokana na mapendekezo nitakayopewa nitayagawa kwenu. Mjipange vizuri kugawiwa kwenu isije kuwa chanzo cha kupigana, mtumie uongozi mlio nao kila mmoja apate kipande, kutakuwa sehemu ya wafugaji na wakulima sababu wote tunategemeana,” amesema Rais Magufuli.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI ONLINE & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!