Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgogoro: Nyumba, mbuzi vyachomwa moto
Habari Mchanganyiko

Mgogoro: Nyumba, mbuzi vyachomwa moto

Spread the love

NYUMBA ya Tryphone Jeremiah, mkazi wa kijiji Kijiji cha Kishanda B, kilichopo kwenye Kata ya Kibale, Kyerwa mkoani Kagera imechomwa moto. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).  

Pia wanyama wake wameuawa pamoja na migomba, mikahawa yake kukatwakatwa. Waliofanya tukio hilo ni wanakijiji wenzake kutokana na mgogoro wa ardhi.

Taarifa zaidi kutoka kijijini humo zinaeleza, wanakijiji hao zaidi ya 250 walifanya tukio hilo Jumapili wiki iliyopita.

“Wanalalamika kwamba namiliki ardhi kubwa,” amesema Jeremiah akieleza mgogoro wake na wanakijiji wenzake “wamevamia shamba na kufyeka mazao zaidi ya hekta 10.5, wameua mbuzi wangu na kuwachoma moto.”

Amesema, mgogoro wake na wananchi ulianza mwaka 2007 kwa baba yake ambaye alilalamikiwa kumiliki ardhi hiyo. Wakati wanakijiji hao wakifanya uharibifu huo, wachungaji walikimbia kukwepa kuuawa.

Ahmed Msengi, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ameeleza, mazao ya kahawa, migomba na miti vimeharibiwa vinaya na wananchi hao.

Medius Atanas, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kishanda B amesema, wanakijiji wamekuwa wakilalamikia Jeremiah kumilikisha ardhi kubwa.

Amesema, wanalalamika kumiliki ardhi ambayo si yake hivyo aliamua kufanya vurugu kwa kuchoma nyumba yake, kuua mifugo jambo ambalo halikubaliki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!