Khamis Mgeja, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga

Mgeja abeza ‘panga pangua’ ya CCM

KHAMIS Mgeja, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na kabla ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema hakuna jipya katika mabadiliko yaliyofanywa na CCM siku nne zilizopita, anaandika Mwandishi wetu.

Mgeja amewambia wanahabari mkoani Tabora kuwa CCM ni ile ile, watu ni wale wale na mambo yake ni yale yale na kwamba wananchi na wanachama wa chama hicho wasitarajie mabadiliko makubwa.

“Kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini naona CCM inajidhoofisha yenyewe bila wao kujua na ninawapa pole sana wajumbe wa NEC-CCM waliopitisha maazimio ya kupunguzwa kwa wajumbe wa kikao hicho kutoka 388 hadi 158.

“Sisi wanachama tuliokuwemo ndani ya CCM muda mrefu tunaweza kufananisha maazimio hayo na kuku kujinyonyoa manyoya yake mwenyewe. Ni mabadiliko ni ya ajabu ambayo hayajawahi kutokea
tangu wakati wa TAA na TANU,” amesema.

Mgeja amedai kuwa nafasi mbalimbali zimefutwa bila hata ya jumuiya za chama kushirikishwa na kwamba suala hilo linaweza kuzua mgawanyiko na hasira za chinichini.

Amesema mabadiliko hayo ni kielelezo cha ukandamizaji wa demokrasia hata ndani ya chama hicho na kuonesha kuwa CCM ina wenyewe ambao wanaweza kuamua jambo lolote.

“Watanzania walitegemea waone mabadiliko ya tunaenda wapi kisiasa na kiuchumi, msimamo halisi ni ujamaa au ubepari? Je, uchumi tunaojenga wa viwanda ni wa kijamaa au wa kibepari lakini pia suala la Katiba mpya na ugumu wa maisha ya watanzania.

Wanafunzi wengi wa vyuo kukosa mikopo, mikataba ya madini, gesi na mafuta kufumuliwa na kuwekwa wazi. Haya ndiyo mambo ya msingi tulitegemea yazungumzwe na chama tawala na watoke na dira ya utekelezaji pamoja na maazimio,” amaesema.

Kuhusu uteuzi wa Humphrey Polepole Katibu wa NEC- Itikadi na Uenezi Mgeja amesema hajui wamemtoa wapi na kudai ni mwanachama mchanga wa chama hicho na labda sifa aliyonayo ni kuwahi kumtukana Edward Lowassa.

“Vijana tangu zamani ndani ya CCM kila aliyemtukana Lowassa alipewa cheo, nadhani Polepole naye amejipatia nafasi hiyo kutokana na juhudi kubwa za kumshambulia Lowassa katika uchaguzi wa mwaka jana,” amesema.

Aidha Mgeja amesema Polepole amejipambanua katika msimamo wa serikali tatu na bado amekubali kuwa mtumishi wa CCM, ambayo msimamo wake ni serikali mbili. Mtu huyu kukubali kuwa mtumishi wa CCM ni kusaliti watanzania kwani alikuwemo katika Tume ya Jaji Joseph Warioba na alipinga CCM kwa kuchakachua maoni ya wananchi.

Amesema Polepole hatoshi kushikilia nafasi hiyo na kwamba pengine nafasi hiyo ingemfaa Charles Mwijage, waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.

KHAMIS Mgeja, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na kabla ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema hakuna jipya katika mabadiliko yaliyofanywa na CCM siku nne zilizopita, anaandika Mwandishi wetu. Mgeja amewambia wanahabari mkoani Tabora kuwa CCM ni ile ile, watu ni wale wale na mambo yake ni yale yale na kwamba wananchi na wanachama wa chama hicho wasitarajie mabadiliko makubwa. “Kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa hapa nchini naona CCM inajidhoofisha yenyewe bila wao kujua na ninawapa pole sana wajumbe wa NEC-CCM waliopitisha maazimio ya kupunguzwa kwa wajumbe wa kikao hicho kutoka 388 hadi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On Youtube