Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (wa pili kushoto) akizindua rasmi huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-hakiki' ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliani Tanzania (TTCL), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba

Mfumo wenye neema kwa wakulima wazinduliwa Tanzania

Spread the love

WAZIRI wa Kilimo wa Tanzania, Japhet Hasunga amezindua rasmi huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la ‘T-hakiki.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu …(endelea).

T-Hakiki ni mfumo wa njia ya simu ambapo unabofya *148*52# na kuingiza namba zilizo kwenye sehemu yenye kivuli kwenye vifungashio vya mbegu au kwenye chupa za viuatilifu ili kuthibitisha uhalisia wa pembejeo.

Uzinduzi wa huduma hiyo inayolenga kuwakomboa wakulima katika mapambano dhidi ya mbegu na viuatilifu feki, umefanyika jana IJumaa tarehe 7 Agosti 2020 ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Hasunga alisema, uuzaji wa pembejeo feki za kilimo umesababisha athari kubwa kijamii na kiuchumi.

“Matokeo yake yamesababisha changamoto nyingi kwa sekta ya kilimo ambayo ndiyo sekta muhimu inayochangia kuongeza tija kwenye uchumi wa Taifa, kwa maana hiyo huduma hii ni mkombozi halisi kwa wakulima wetu,” alisema Hasunga.

Alisema huduma hiyo imetokana na ubunifu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwa kushirikiana na Kampuni ya Quincewood Group Limited na wadau wa sekta ya kilimo kama vile Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) na Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa Viuatilifu (TPRI), ambao sasa wamekuja na suluhisho la kiteklonojia kukomesha matumizi ya pembejeo feki.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa TPRI, Dk. Margaret Mollel alisema, ubunifu huo umeenda sambamba na malengo ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngwediagi alisema huduma hii itamsaidia mkulima kufahamu matumizi sahihi ya pembejeo hizo kupitia simu ya mkononi, hakika haya ni mapinduzi bora ambayo yatazidi kumkomboa mkulima lakini pia kuisaidia Serikali kukabiliana na wafanyabiashara wa pembejeo wasio waadilifu.

“T-Hakiki itaboresha sekta ya kilimo na italinda maisha ya wakulima wengi katika kuendesha shughuli za kilimo na kulinda thamani ya fedha zao,” alisema.

Aidha, akifafanua namna mfumo huo unavyofanya kazi, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema T- Hakiki ni huduma ya simu ya mkononi ambayo ni mkombozi kwa sekta ya kilimo nchini, pia inalinda maisha ya wakulima wengi kwa kuongeza usalama wa chakula nchini Tanzania.

Alisema teknolojia hiyo inakusudia kufungua ukurasa mpya kwa wakulima kwa kuja na suluhisho ambalo linapatikana kirahisi.

Kindamba alisema, kwa sababu huduma hiyo itawasaidia wakulima kutambua pembejeo feki na kuzitolea taarifa kama hatua mojawapo ya kukomesha matumizi ya pembejeo feki.

Alisema, huduma hiyo inapatikana katika mitandao yote ya simu na ni bure.

WAZIRI wa Kilimo wa Tanzania, Japhet Hasunga amezindua rasmi huduma maalum ya kuhakiki pembejeo inayofahamika kwa jina la 'T-hakiki.' Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu …(endelea). T-Hakiki ni mfumo wa njia ya simu ambapo unabofya *148*52# na kuingiza namba zilizo kwenye sehemu yenye kivuli kwenye vifungashio vya mbegu au kwenye chupa za viuatilifu ili kuthibitisha uhalisia wa pembejeo. Uzinduzi wa huduma hiyo inayolenga kuwakomboa wakulima katika mapambano dhidi ya mbegu na viuatilifu feki, umefanyika jana IJumaa tarehe 7 Agosti 2020 ndani ya Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), kwenye Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. Hasunga alisema,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!