Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mfumo wa GePG mwarobaini kwa ‘wapiga dili’
Habari za SiasaTangulizi

Mfumo wa GePG mwarobaini kwa ‘wapiga dili’

Bomba la maji safi
Spread the love

MAMLAKA ya Maji safi na usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mkoani Mwanza imesema kuwa mfumo mpya wa kielektroniki wa malipo ya serikali wa GePG umesaidia kupunguza upigaji wa fedha za umma uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Imesema mfumo huo umesaidia pia upatikanaji wa ankara na kufanya malipo haraka kwa wananchi pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa na kuongeza mapato kwa idara mbalimbali na taasisi za serikali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja Biashara wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (Mwauwasa) mkoani hapa, Meck Manyama wakati wa uzinduzi rasmi wa ulipaji wa ankara za maji kupitia simu ya mkononi ya kampuni ya Tigo kwa mikoa ya kanda ya ziwa.

Manyama ambaye alimwakilisha mkurugenzi wa Mwauwasa Antony Sanga, amesema kwa sasa  wateja wa tigo katika mikoa hiyo, wanaweza kufanya malipo kwa kutumia mfumo huo mpya unaotoa huduma kwa wakati muafaka.

Manyama amesema kwa sasa wananchi na watumiaji wa Tigo wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka Mwauwasa hatua ambayo alidai itazidi  kurahisisha ukusanyaji wa mapato.

“Baadhi ya taasisi za serikali ambazo malipo yao yanaweza kufanywa na tigo pesa ni Wizara ya ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mamlaka za miji na Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA)  pamoja na mashirika mengine na idara nyingine zaidi ya 300.

“Pamoja na hayo ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo pesa  mfumo (app) na Qr Code, wateja wa tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo pesa na kuscan QR code kasha kuweka namba ya siri ili kufanikisha muamala,” amesema Manyama.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tigo kanda ya ziwa, Athuman Madati amesema wameamua kuzindua na kuongeza malipo ya serikalini kwenye orodha ya Tigo Pesa kuwafanya wateja wao kufurahia huduma zao zaidi.

“Kuanzia leo wateja wa kampuni ya Tigo wanaweza kulipa bili kwa kutumia mfumo wa kielektroniki wamalipo serikalini (GePG) pia wateja wetu zaidi ya milioni saba wana uwezo wa kufanya malipo kwa haraka kwenye taasisi, wizara, wakara wa serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo pesa USSD, Tigo pesa App na QR code,” amesema Madati.

Kufahamu deni la maji na usamoja wa mita (mteja) anashauriwa kuingia kwenye simu yake ya mkononi na kupiga *150* 00# ambapo hapo utaletewa deni unalodaiwa na mamlaka husika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!