Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mfanyabiashara Tunduma aigomea CCM, abambikiwa makesi lukuki 
Habari za SiasaTangulizi

Mfanyabiashara Tunduma aigomea CCM, abambikiwa makesi lukuki 

Spread the love

MFANYABIASHARA maarufu mjini Tunduma, Isakwisa Thobias Lupembe, anatuhumiwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Songwe, kuwa sio raia wa Jamhuri ya Muungano; huku akihusisha na masuala ya kisiasa. Anaripoti Kenneth Ngeles … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari, mjini Tunduma, Isakwisa alisema, sababu za kuhusisha tuhuma zake na siasa zinatokana na yeye kufuatwa na baadhi ya viongozi Chama Cha Mapinduzi (CCM), mapema mwaka jana na kumtaka kuhamia chama hicho. Hakutaka kuwataja waliomshawishi kuhamia chama hicho na kukiacha chama chake anachokipenda CHADEMA.

Anasema, baada ya kuonyesha msimamo wake wa kutokubaliana na mjumbe huyo, alianza kupata taarifa kutoka kwa baadhi ya rafiki zake wa karibu ambao ni wafuasi wa CCM kuwa kitakachofuata ni kufilisiwa kila kitu.

Isakwisa (43), ni mzaliwa wa kitongoji cha Ntundumbaka kijiji cha Lusungo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Anasema, baada ya kuweka msimamo kuwa hayupo tayari kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ndipo mikasa ilipoanza kumuandama.

Kwanza, mfanyabiashara huyo anasema, “walikuja watu kutoka mamlaka ya mapato (TRA). Wakanieleza nadaiwa kodi ya kiasi cha Sh. 370 milioni na kwamba zijaweza kulipa kodi ya serikali kwa kipindi cha miaka mitatu.”

Isakwisa ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Crasical Enginering Limited, iliyokuwa ikihusisha na ukusanyaji wa ushuru wa mazao anasema, wakati suala hilo bado halijaisha, halmashauri ya Mji wa Tunduma ilivunja mikataba yote ya kukusanya ushuru.

“Walianza TRA, kwamba nadaiwa kodi ya Sh. 337 milioni ambayo haiendani kabisa na biashara yangu. Baadaye wakaja Halmashauri ya Mji Tunduma, ambayo ilivunja mikataba na kampuni yangu ya kukusanya ushuru katika vyanzo vya mapato bila kurejesha bondi yangu ya Sh. 80 milioni. Nimewashitaki na kesi inaendelea mahakamani,” anaeleza.

Anasema, “linalo nisikitisha na kuniumiza sana, ni hili la uhamiaji. Wameshaniita zaidi ya mara tatu, kwamba wana mashaka na uraia wangu. Wote hawa, ukikaa nao pembeni na kuwahoji, wanakwambi nia agizo la kamati ya ulinzi na usalama; na mara nyingine, watakwambia masuala yenu ya siasa.”

Isakwisa alikuwa ndiye wakala wa mwisho wa mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mbomba, ni mkuu wa wilaya hiyo, Juma Irando.

“Tuhuma zote nazielekeza kwa mkuu wa wilaya na haya yote yanafanyika kwa maagizo yake kwa lengo la kunidhofisha kiuchumi kwani wao wanaamini kuwa nguvu ya Chadema ipo mikoni mwangu,” anaeleza.

Akizungumzia adhari anazopota hasa kwa tuhuma za urai wake, Isakwisa anasema, maisha yake yapo hatarini kwani haaminiki tena na jamii ambayo anayoishi. Anasema amekuwa katika mji wa Tunduma tokea mwaka 2000, alipofika akitokea wilayani Kyela.

Anasema, “maisha yangu yapo hatarini. Jamii hainiaamini tena, lakini pia shughuli zangu za kiuchumi haziendi kama ilivyokuwa hasa kutokana na hofu iliyopo katika jamii yangu inayonizunguka.”

Kwa upande wake, mzazi wa Thobias Syagee Lupembe (76) anasema, amesikitishwa na tuhuma zinazo mkabali mwanaye huyo ambaye ni wa sita kati ya watoto nane aliyojaliwa na mkewe Teresia Rudhati Mahundi.

“Kwa kweli, sisi kama wazazi tunaumizwa na kusikitishwa kwa tuhuma hizi dhidi ya mwanetu. Lakini yote tunamwachia Mungu,” ameeeza Mzee Thobais kwa sauti ya masikitiko.

Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Kanani, Timotheo Mwamlima anasema, suala la Isakwisa kuitwa sio raia, limewashtua wengi kutokana na ukweli kuwa madai hayo hayana ukweli.

Mwandishi wa habari hizi alilifika makao makuu ya uhamiaji mkoa wa Songwe na kukutana na Kaimu kamanda wa Uhamiaji, Mariam Mwanzaliama ambaye aligoma kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa yeye sio msemaji wa idara hiyo.

“Siwezi kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo. Mimi siyo msemaji. Mkuu hayupo lakini pia ofisi za uhamiaji Tunduma, wakati fulani masuala yao wanawajibika moja kwa moja makao makuu,” alieleza Mwanzaliama.

Kwa upande wake Meneja TRA mkoa wa Songwe, Paul Walalaze, alikiri kuwepo kwa suala la Isakwisa mezani kwake. Alikana madai kuwa suala hilo linahusiana na mambo ya kisiasa.

“Suala hilo lipo na siyo kodi … ni kwamba hivi tulifanya ni kumpa oda ya kuwa anadaiwa kiasi hicho cha fedha na hii kutokana na kodi anazo lipa hazingaa mtiririko ya fedha katika akaunti zake; hivyo alichotakiwa kufanya ni kuja na mshauri wake na kutoa mchanganuo wa mapato yake,” ameeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!