Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mfanyabiashara pombe kali, wenzake wafikisha kortini
Habari Mchanganyiko

Mfanyabiashara pombe kali, wenzake wafikisha kortini

Spread the love

MFANYABIASHARA wa pombe kali na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jaluma General Suppliers Limited Lucas Mallya na wenzake wanane, wamefikishwa mahakamani kwa makosa 28 yakiwemo uhujumu uchumi,kushirikiana na magenge ya uhalifu na kukwepa kodi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Watu hao wamefunguliwa mashtaka hayo katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam leo tarehe 29 Januari 2020.

Wakisomewa mashtaka na Faraji Nguka, Wakili wa Serikali Mwandamizi,  akisaidiana na Zacharia Ndaskoi, mbele ya Godfrey Isaya, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, watuhumiwa wote kwa pamoja wanadaiwa katika nyakati tofauti kati ya tarehe 1 Januari 2015, hadi tarehe 7 Januari 2020, Dar es Salaam, kwa makusudi, waliongoza genge la uhalifu.

Nguka amedai, katika kosa la kughushi nyaraka za ‘electronic tax stamp’, mtuhumiwa namba moja Lucas Mallya, alitengeneza nyaraka hizo kati au kabla ya mwaka jana jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kughushi na kuonesha kuwa, zimetengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitu ambacho si cha kweli.

Shtaka la pili linalomkabili Mallya ni, kuwasilisha nyaraka za uongo ambapo inadaiwa, kati ama kabla ya tarehe 3 Juni 2019, jijini Dar es Salaam, kwa kujua na kukusudia, alitoa nyaraka zikiwemo stakabadhi za malipo kwa TRA, akidai kuwa ni nyaraka halisi ilhali akijua ni za kughushi.

Shtaka la tatu linalomkabili Mallya ni, kupatikana na tempu za ushuru bila Kibali, inadaiwa kuwa tarehe 7 January 2020 eneo la Chanyang’ombe Temeke jijini Dar es Salaam, alikuwa akimiliki mabunda 93 ya tempu za kieletroniki za ushuru zenye thamani ya Shilingi 80.5 Milioni, zilizochapishwa bila idhini ya Kamshna wa TRA.

Shtaka la nne kwa mtuhumiwa Mallya ni, kuisababishia Mamlaka ya Mapato hasara kiasi ya Shilingi 15.2 Bilioni, ambapo anadaiwa kati ya tarehe 1 Januri 2016 na tarehe 31 Desemba 2019, ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa kukusudia alighushi stampe za TRA na kuisababisha hasara hiyo Serikali.

Shtaka la tano linamkabili mshtakiwa Mallya ni la kukwepa Kodi, ambapo anaidaiwa kati ya tarehe 1 Januri 2016 na tarehe 31 Desemba 2019, kwa kusudi la kukwepa kodi alitengeneza mabunda 93 ya Tempu za kieletroni za ushuru, na kukwepa kulipa kodi yenye thamani ya Shilingi 15.2 Bilioni.

Katika shtaka la sita, Mallya anadaiwa kutakatisha fedha kiasi cha shilingi 15.2 Bilioni ambapo anadaiwa kutekeleza kitendo hicho tarehe 1Januri 2016 na tarehe 31 Desemba 2019, ndani ya jiji la Dar es Salaam huku akijua kuwa pesa hizo ni mazalia ya uhalifu.

Mshtakiwa kwenye shauri hilo Mfanyabiashara Emmanuel Vincent (25) , anakabiliwa na kosa la kukutwa a Tempu za ushuru bila idhini ya Mamlaka ya Kamishna wa TRA, ambapo anadaiwa kukutwa na stempu hizo tarehe 3 Januari 2020, zenye thamani ya Shilingi 1 Milioni.

Mshtakiwa wa tatu ni, Happy Peter ambaye ni Mkurugenzi wa Happy Import Associate, anashtakiwa mahakamani  hapo kwa kuingiza bila kibali bidhaa zenye thamani ya shilingi 24 Milioni.

Anadaiwa kati ya January 1 2017, na Desemba 31 2019,   ndani ya jiji la Dar es Salaam, aliingiza bidhaa hizo bila kusajiliwa na  kamishna TRA.

Happy anakabiliwa na shtaka la kukwepa kodi, ambapo kati ya January 1, 2017 na Desemba 31, 2019, jijini Dar es Salaam kwa kusudi la kukwepa kulipa  kodi, aliingiza bidhaa bila kusajili zenye thamani ya shilingi Bilioni 9.5. Iliyopaswa kulipwa TRA.

Pia, Happy anadaiwa kuingizia hasara serikali kiasi cha shilingi Bilioni 9.5,  ambapo tarehe 1 January 2017 na tarehe 31 Desemba 2019, ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa makusudi aliingiza na kusambaza bidhaa bila leseni kwa kutumia tempu za kughushi na kuisababisha hasara Serikali.

Shtaka jingine kwa mshtakiwa Happy ni, utakatishaji fedha ambapo inadaiwa tarehe 1Januri 2017 na tarehe 31 Desemba 2019, alitakatisha fedha kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 ilhali akijua ni zao uhalifu .

Mshtakiwa mwengine ni, Procheses Shayo na Prokokolini Shayo, wanakabiliwa na shtaka la kusambaza bidhaa bila kuwa na Kibali,  zenye thamani ya shilingi million 139.

Na kushindwa kulipa kodi  kiasi cha shilingi milioni 38, pamoja na kuisababishia Serikali hasara kiasi cha shilingi million 38 kati au baada ya tarehe 19 Desemba 2019 .

Shtaka jingine linalomkabili Procheses Shayo, ni kushindwa kulipa kodi na kuisababisha Serikali hasara ya Shilingi Bilioni 2.3, kati ya tarehe 1Desemba 2019 na Tarehe 31 Desemba 2019.

Godfrey Ulio ambaye ni Mkurugenzi wa GMU Group Company Limited, amesomewa shtaka la kukwepa kodi na kuisababishia hasara na kutakatisha fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.2, ambapo anadaiwa kutekeleza hayo  kati ya tarehe 1 Januari 2015, na Desemba 31 2018 jijini, Dar es Salaam.

Tunsubilege Mateni, ambaye ni mhasibu 3D’s Accounts Consultant na Nelson Kahangwa, Mkaguzi wa Diamond Financial Services, wanashtakiwa kwa kosa la kuandaa hati ya uongo kati ya tarehe 1 Januari 2015 na mwezi Desemba 2018 jijini Dar es Salaam.

Kwa pamoja wanadaiwa  kutengeneza nyaraka ya uongo, ambapo ni ripoti ya mapato ya kampuni ya GMU, kwa mwaka mapato ya 2015/2016 na 2017,  kwa kusudi kujinufaisha.

Shtaka linalowakabili Mateni na Kahangwa ni kusaidia kufanya uhalifu,  ambapo wanadaiwa kati ya tarehe 1 Januari 2015 na tarehe 31 Disemba 2018,   kwa kuandaa nyaraka ya mapato kwa ajili ya kumsaidi Godfrey Ulio,  kukwepo kodi.

Shtaka jingine kwa Mateni na Kahangwa ni, kutakatisha fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.2. Wanadaiwa kufanya kitendo hicho kati ya tarehe 1 Januari 2015,  na tarehe 31 Desemba 2018, huku wakijua ni matokeo ya uhalifu.

Nyasulu Eneck,  amesomewa shtaka la kushindwa kulipa kodi kiasi cha shilingi million 89, na kushindwa kutoa risiti za kieletroniki, baada ya kutolea malipo yenye thamani ya Shilingi Milioni 98 kutokana na kuuza bidhaa.

Enock anakabiliwa na kosa la kuongoza bidhaa bila kusajiliwa.

Anadaiwa kati ya tarehe 23 Desemba 2019 jijini Dar es Salaam, aliingiza bidhaa za vinywaji vya pombe kali venye thamani ya Shilingi Milioni 95,  bila kusajili.

Enock anashtakiwa kwa kuisababishia mamlaka hasara kiasi cha shilingi million 89, kutokana kuingiza bidhaa bila kusajiliwa na kukwepa kodi.

Enock anakabiliwa na shtaka la utakatishaji fedha haramu ambapo anadaiwa kutakatisha kiasi cha shilingi milioni 89, kwa kujipatia fedha hizo akijua ni zao la uhalifu.

Baada ya kusoma mashtaka hayo wakili Nguka amedai uchunguzi wa mashtaka hayo bado haujakamilika.

Na Hakimu Isaya ameahirisha shauri hilo hadi tarehe 12 February mwaka huu, na kuwataka washtakiwa hao kutojibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!