Mfalme wa Japan, Akihito

Mfalme wa Japan ang’atuka mwenyewe

MFALME wa Japan, Akihito (85) ameng’atuka katika wadhifa huo baada ya kutawala kwa miongo mitatu, kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Mfalme Akihito ameachia ngazi jana tarehe 30 Aprili 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na mtoto wake, Naruhito.

Mfalme mpya, Naruhito anayetarajiwa kukasimishwa mamlaka ya ufalme leo Jumatano tarehe 1 Mei 2019, anaanza majukumu yake rasmi kwa mujibu wa katiba na sheria za Japan.  

Mfalme Naruhito wakati akiapa, aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba na sheria za taifa hilo.

Mfalme aliyemaliza muda wake, Akihito alishukuru wananchi wa Japan  na kuwahimiza kuendelea kuienzi amani.

MFALME wa Japan, Akihito (85) ameng’atuka katika wadhifa huo baada ya kutawala kwa miongo mitatu, kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Mfalme Akihito ameachia ngazi jana tarehe 30 Aprili 2019 na nafasi yake kuchukuliwa na mtoto wake, Naruhito. Mfalme mpya, Naruhito anayetarajiwa kukasimishwa mamlaka ya ufalme leo Jumatano tarehe 1 Mei 2019, anaanza majukumu yake rasmi kwa mujibu wa katiba na sheria za Japan.   Mfalme Naruhito wakati akiapa, aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba na sheria za taifa hilo. Mfalme aliyemaliza muda wake, Akihito alishukuru wananchi wa Japan  na kuwahimiza kuendelea kuienzi amani.

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram