Meya wa zamani wa Manispaa ya Kinondoni Alhaji Salum Londa

Meya Londa ajisalimisha Urafiki

Spread the love

ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Alhaji Salum Salehe Londa, amelipa deni la pango ya nyumba, analodaiwa na kiwanda cha Nguo cha Urafiki, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa kutoka ndani ya shirika hilo zinasema, Londa alifika makao makuu ya kiwanda hicho yaliyopo maeneo ya Urafiki, barabara ya Morogoro, Ubungo jijini Dar es Salaam, majira ya saa tisa jioni ya leo Jumatano kulipa deni lake.

Londa anadaiwa na kampuni hiyo kiasi cha Sh. 18 milioni ikiwa ni pango la nyumba anayoishi iliyopo eneo la Makaburini, Kinondoni.

Mwandishi wa habari hii, alikutana na Londa ndani ya kiwanda hicho akielekea sehemu ya malipo ili kulipa deni lake.

Habari zinasema Meya Londa amelipa fedha zote Sh. 18 milioni alizokuwa anadaiwa na kiasi gani katika deni analodaiwa na kampuni ya Urafiki.

Awali taarifa zinasema, kampuni hiyo kupitia wakala wake wa kukusanya madeni – Yono Action Mart – ilitoa hadi saa tisa jioni ya leo kwa mwanasiasa huyo wa zamani kulipa deni, vinginevyo angefukuzwa kwenye nyumba hiyo.

ALIYEKUWA Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Alhaji Salum Salehe Londa, amelipa deni la pango ya nyumba, analodaiwa na kiwanda cha Nguo cha Urafiki, anaandika Hamisi Mguta. Taarifa kutoka ndani ya shirika hilo zinasema, Londa alifika makao makuu ya kiwanda hicho yaliyopo maeneo ya Urafiki, barabara ya Morogoro, Ubungo jijini Dar es Salaam, majira ya saa tisa jioni ya leo Jumatano kulipa deni lake. Londa anadaiwa na kampuni hiyo kiasi cha Sh. 18 milioni ikiwa ni pango la nyumba anayoishi iliyopo eneo la Makaburini, Kinondoni. Mwandishi wa habari hii, alikutana na Londa ndani ya kiwanda hicho akielekea sehemu ya malipo ili…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Hamisi Mguta

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!