Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mussa Kafana

Meya Dar: Ngoma ngumu 2020

USHINDI wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenye uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam ni ishara kwamba uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa pamoja na Uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa utakuwa mgumu zaidi, anaripoti Faki Sosi… (endelea).

Hayo yamezungumzwa leo na Naibu Meya wa jiji Mussa Kafana aliyeshinda katika uchaguzi huo uliofanyika juzi Januari 4 Mwaka huu alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online .

”Uchaguzi wa Mdogo wa Mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hautakuwa rahisi…. chochote kinaweza kutokea, yoyote anaweza kuingia Ikulu” amesema.

Kafana ambaye ni Diwani wa Kiwalani (CUF) ameeleza kuwa  ushindi wa ukawa ulikuwa ni wa lazima kwa sababu ufanisi wake uliwashawishi madiwani wote ambapo angeweza kushinda nafasi hiyo hataka wapiga kura wa ukawa wangekuwa kidogo angeshinda kwenye nafasi hiyo.

Licha ya hapo awali familia kutaka kumzuia Kafana asipelekwe kushiriki uchaguzi huo kutokana na kuwa alikuwa mgonjwa amesema hakukuwa na njia nyingine ya kutetea ushindi wake zaidi ya kushiriki uchaguzi huo akiwa hoi.

Kafana amesema CCM wasiumize kishwa kumtafuta nani aliyepigia kura upinzani hadi kupelekea ushindi wake kwani unatokana na uwaminifu wake alionesha alipopewa  nafasi hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2015/2016 na kwamba madiwani wa vyama vyote alishirikiana nao hivyo aliamini CCM watampigia kura kutokana na ufanisi wake.

“Ukawa haukutikisika pamoja na kuibuka kwa matatizo ndani ya vyama vinavyounda ukawa kama vile madiwani kununuliwa , mgogoro ndani ya CUF lakini umoja wetu bado uko vizuri” amesema.

USHINDI wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwenye uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam ni ishara kwamba uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa pamoja na Uchaguzi mkuu wa 2020 kuwa utakuwa mgumu zaidi, anaripoti Faki Sosi… (endelea). Hayo yamezungumzwa leo na Naibu Meya wa jiji Mussa Kafana aliyeshinda katika uchaguzi huo uliofanyika juzi Januari 4 Mwaka huu alipokuwa akizungumza na MwanaHALISI Online . https://www.youtube.com/watch?v=kBXGTkwlmjo ''Uchaguzi wa Mdogo wa Mwaka 2019 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hautakuwa rahisi.... chochote kinaweza kutokea, yoyote anaweza kuingia Ikulu'' amesema. Kafana ambaye ni Diwani wa Kiwalani (CUF) ameeleza kuwa  ushindi…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Faki Sosi

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram