Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Meya Dar: Maji yamenifika shingoni
Habari za Siasa

Meya Dar: Maji yamenifika shingoni

Spread the love

ISAYA Mwita, Meya wa Jiji la Dar es Salaam anaonekana kukata tamaaa, ni baada ya kuundiwa kamati ya kuchunguza kuhusu tuhuma zinazomkabili. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Akizungumza na kituo cha Redio cha East Africa mtandaoni leo tarehe 6 Januari 2019, Mwita ameeleza, haoni mwanga mbele bali giza nene, na kwamba kilichobaki ni kumwachia Mungu.

Mwita anatuhumiwa kutotumia Sh5.8 bilioni za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), matumizi mabaya ya gari ya ofisi, kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani pia kupendelea baadhi ya mameya kuingia katika kamati za fedha.

Amesema, tuhuma anazobebeshwa nazo na hata kusababisha Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuunda kamati ya kumchunguza, hazina ukweli wowote.

“Kiukweli sasa maji kwangu yapo shingoni, mbele sioni wala nyuma sioni ila naamini Mwenyezi Mungu atasimama,” amesema Mwita.

Akizungumzia kisa cha kubebeshwa tuhuma hizo Mwita amedai, tatizo lilianzia kwenye matumizi ya pesa za UDA, “pesa hizo hatukuzitumia kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi, sasa nimeshangaa ambao tulikubaliana kutozitumia wananilalamikia mimi,” amesema.

Kuhusu tuhuma za matumizi mabaya ya gari la ofisi, Isaya amesema, dereva wake alisababisha ajali katika eneo la Ubungo na kwamba kwa kuwa wanamsakama, wameshikilia suala hilo kuwa matumizi mabaya ya gari hilo.

“Dereva wangu alisababisha ajali katika eneo la Ubungo, kwa hiyo madiwani wamelalalamikia mimi nimetumia chombo cha moto vibaya, yaani wamenikalia kooni kweli,” amesema na kuongeza;

“Umeya wangu sasa unapimwa ikiwa imebaki miezi mitatu kabla hatujavunja Baraza la Madiwani, na hivi karibuni nimeanza kupata wakati mgumu kwenye kiti changu, naomba masheikh na viongozi wengine wa dini waniombee.”

Mwita ambaye ni diwani wa Vijibweni (Chadema) na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliyechaguliwa mwaka 2016.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!