Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe: Niko tayari kugombea urais Tanzania, Chadema…
Habari za Siasa

Membe: Niko tayari kugombea urais Tanzania, Chadema…

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo
Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje nchini Tanzania amekubali ombi la wanachama wa ACT-Wazalendo la kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi, Dar es Salaam…(endelea)

Membe ametoa kauli hiyo leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 ikiwa ni siku moja kupita tangu alipopokelewa rasmi ndani ya ACT-Wazalendo jana Alhamisi katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo amejiunga na chama hicho cha upinzani baada ya kufukuzwa ndani ya chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) alichokulia kwa kile kilichoelezwa hakuwa na mienendo inayoridhisha tangu mwaka 2014.

Wanachama wa ACT-Wazalendo, wakiwa kwenye mkutano Mlimani City

Baada ya kupokelewa na wanachama pamoja na viongozi waandamizi wa ACT-Wazalendo wakiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe, mwanasiasa huyo aliombwa agombee urais.

Maalim Seif ambaye amekwisha kuchuklua na kurejesha fomu ya kuwania urais Zanizbar alisema, wanachama wa chama hicho wamemtuma amweleze Membe agombee urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Soma zaidi hapa

Maalim Seif: Membe unaogopwa, gombea urais Tanzania

Leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020, kupitia akaunti yake ya kijamii ya Twitter, Membe ameandika, “jana niliombwa na leo nimekubali rasmi kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo.”

“Huu ni wakati muafaka kwangu wa kushiriki katika mazungumzo na vyama vingine kama Chadema ili tusimamishe “KISIKI CHA MPINGO” kimoja!.”

Katika mazungumzo yake jana baada ya kupokelewa, Membe aliomba kambi rasmi ya upinzani inayoundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana katika uchaguzi huo ili kuhakikisha wanaiondoa madarakani serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao.

Soma zaidi hapa

Membe akoleza moto urais Tanzania, atoa ombi Chadema

MwanaHALISI Online limezungumza na Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu kuhusu ambaye amesema kuna uwezekano Membe akachukua fomu ya kuwania urais leo Ijumaa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

1 Comment

  • Walitangulia kabla yake lakini wenyewe wamesalim amri anataka kujizalilisha tu hawa ndio wanaotamaa Na madaraka sio uongozi hawana lolote kama wewe no basi ni no hata kama utachinja bahari haitafaa kitu au umwetumwa kukiua hicho chama basi hogera na nyie wa vyama kueni na upeo kila uchaguzi mnarubuniwa na nyinyi hamusoni mtaburuzwa mpaka ? Ifikapo mwaka 2025 tutahamia chama nanihino?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!