Wednesday , 17 April 2024
Habari za SiasaTangulizi

Membe: Naisubiri NEC

Spread the love

SIKU moja baada ya Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuketi jijini Dar es Salaam, Bernard Membe amesema, ‘anasikilizia’ uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kikao hicho cha CC, kilipokea taarifa ya awali ya Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho, ikiwa ni baada Membe ambaye ni Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na makatibu wakuu wastaafu, Yusuf Makamba na Abrahman Kinana kuhojiwa.

Membe ametoa kauli hiyo tarehe 13 Februari 2020, wakati akihojiwa na gazeti moja la kila siku, kuhusu maoni yake juu ya sakata hilo.

Kauli hiyo ya Membe imekuja siku moja baada ya Kamati Kuu ya CCM kutoa siku saba kwa Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu ya chama hicho, kuwasilisha taarifa ya mahojiano yake na Membe, pamoja na Makatibu Wakuu Wastaafu, Mzee Yusuph Makamba na Abdulrahman Kinana, katika mamlaka vikao husika.

Akizungumzia hatua hiyo, Membe amesema anasubiri uamuzi wa NEC kuhusu suala hilo. Huku akiweka wazi kwamba, yuko tayari kupokea uamuzi wowote wa halamshauri hiyo dhidi yake.

“Huu ndio utaratibu, suala la siku ziwe saba au kumi mimi linanihusuje? Mimi nimemaliza sehemu yangu na wao wamepewa muda wamalize sehemu yao. sihitaji kujipanga nipo bize na shughuli zangu nyingine,” ameeleza Membe na kuongeza:

“Ni vizuri kufahamu kuwa NEC, ndiyo itakayotoa uamuzi, kamati kuu itapendekeza tu. tusubiri kikao cha halmashauri kuu. Huu ndio mchakato mnapaswa kujua.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!