Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe kutua Tanzania, asema yuko imara
Habari za Siasa

Membe kutua Tanzania, asema yuko imara

Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, mgombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, anarejea nchini mwake kesho Jumanne tarehe 15 Septemba 2020 akitokea Dubai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Membe aliondoka nchini Tanzania hivi karibuni kwenda Dubai ikiwa ni siku chache kupita tangu alipozindua kampeni zake za urais mkoani Lindi na kufanya mikutano kadhaa mikoa ya Mtwara na Pwani.

Mwanadiplosia huyo mashuhuri aliyepata kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania kuanzia mwaka 2007 hadi 2015, ametumia ukaunti yake ya Twitter kuelezea safari yake.

“Wana ACT- Wazalendo na Watanzania wenzangu wote! kesho Jumanne ya tarehe 15 Sept.saa 8.40 mchana, nitatua DSM nikitokea Dubai na nitafanya Press Conference Airport.”

“Afya yangu imeimarika na sasa nipo tayari kwa kampeni ya Urais inayoanzia Tabora wiki hii hadi 26 Oktoba 26,” ameandika Membe ambaye pia ni Mshauri Mkuu wa ACT-Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!