Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe azidi kuwatega upinzani, asema atashinda urais 2020
Habari za SiasaTangulizi

Membe azidi kuwatega upinzani, asema atashinda urais 2020

Marehemu Bernard Membe enzi za uhai wake
Spread the love

BERNARD Membe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania anazidi kuviweka mtegoni vyama vya upinzani nchini humo baada ya kusema, atagombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 na atashinda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Membe ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 6 Julai 2020 wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa Rondo Mkoa wa Lindi, waliomsindikiza kurejesha kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Tarehe 28 Februari 2020, Kamati Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuzwa uanachama kwa madai amekuwa akikiuka taratibu na miongozo ya chama hicho tangu mwaka 2014.

Tarehe 13 Desemba 2019, Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana jijini Mwanza chini ya Mwenyekiti wake, Rais John Pombe Magufuli ilitoa maagizo kamati ya maadili kuwahoji Membe na makatibu wakuu wastaafu wa CCM,  Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Wakati halmashauri kuu ilitoa maagizo hayo, ililidhia msamaha uliokuwa umekwisha kutolewa na Rais Magufuli dhidi ya wabunge wake watatu, William Ngeleja (Sengerema), Nape Nnauye (Mtama) na January Makamba (Bumbuli).

Msingi wa mahojiano hayo ya sauti zao, yalitanguliwa na waraka wa Kinana na Makamba kuandika tarehe 14 Julai 2019 kwenda kwa Katibu wa Baraza la Wazee la CCM, Pius Msekwa wakidai uongozi hauwalindi dhidi ya mtu ambaye alikuwa akiwadhalilisha na walimwelezea analindwa na mtu mwenye mamlaka.

Waraka huo, ulifuatiwa na sauti za wanachama hao wasambaa mitandaoni wakizungumzia kuporomoka kwa uongozi wa CCM akiwemo Rais Magufuli.

Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM waliomsindikiza ambao nao walirejesha kadi za uanachama, Membe alisema anasubiri mabaraza ya vyama hivyo yaanze kukutana na kujadili sharti hilo ili aamue rasmi atagombea kupitia chama gani.

“Tutajiunga na chama na tutagombea uongozi wa juu wa nchi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu na mwezi wa kumi tutashinda,” amesema Membe huku akishangiliwa

Akiwatuliza wanachama hao, Membe amesema,”Sijakisema chama kwasababu mabaraza ya hivyo vyama yanakutana, sio vizuri tukatangulia kujipa wakati mabaraza yale yanakaa kuanzia sasa kujadili suala la ‘Rondo’ na jibu litakuwa ndio.”

Membe amesema,” Nawaomba tuvumilie masaa tu na siku, sisi tunafuata taratibu na tayari tumeshawaroga na tumepeleka vitu vyetu huko sasa hivi wanakaa kwa starehe.”

Hivi karibuni, Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo akiwa ziarani mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi, alimkaribisha Membe kujiunga na upinzani ili kuendeleza mapambano ya kupigania demokrasia.

Ombi la Membe kwa vyama vya upinzani ni Kutaka kuungana kuwa kitu kimoja kama ilivyofanyika katika uchaguzi wa mwaka 2015 kwa vyama vinne kushirikiana.

Vyama hivyo vilikuwa NLD, NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katika uchaguzi huo, nafasi ya urais walimsimamisha mgombea mmoja,Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kufanikiwa kutoa mchuano mkali kwa CCM.

Hata hivyo, Lowassa na Ukawa kwa jumla walipata kura milioni sita sawa na asilimia 39 za kura zote milioni 15 zilizopigwa huku Dk. John Pombe Magufuli wa CCM akiibuka mshindi kwa kupata kura milioni nane sawa na asilimia 58 ya kura hizo.

Lowassa aliyejiunga na upinzani tarehe 28 Julai 2015 baada ya jina lake kukatwa katika mbio za urais ndani ya CCM, tarehe 1 Machi 2019, Lowassa alirejea CCM na kupokewa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiweno Rais Magufuli ofisi za Lumumba, Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!