Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amteua Membe kuwa mshauri mkuu ACT-Wazalendo
Habari za Siasa

Zitto amteua Membe kuwa mshauri mkuu ACT-Wazalendo

Bernard Membe
Spread the love

BERNARD Membe, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo, amepewa cheo cha ‘mshauri wa chama’ hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kabla ya Membe, cheo hicho kilikuwa cha Maalim Seif Sharif Hamad, ambapo baada ya kugombea na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, nafasi ya mshauri wa chama ilibaki wazi.

Zitto Kabwe, kiongozi wa chama hicho ndiye aliyependekeza cheo hicho kwa Membe kwenye kikao cha wajumbe wa Halmashuri Kuu kinachofanyika leo tarehe 3 Agosti 2020, katika Ukumbi wa Mikutano wa Lamada jijini Dar es Salaam.

“Kuna nafasi zilizo wazi, miongoni mwazo ni nafasi ya mshauri wa chama, hivyo tunapendekeza Bernard Membe kuwa mshauri mkuu wa chama chetu,” Zitto aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho.

Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo

Wajumbe hao walipokea kwa shangwe pendekezo hilo, huku wakipiga makofi kupongeza hatua ya Membe kupendekezwa kuwa mshauri wa chama hicho.

“Mheshimiwa mwenyekiti (Maalim Seif), kwa makofi na shangwe hizi, naona wajumbe wa Halmashauri Kuu wameridhia Membe kuwa mshauri wa chama chetu,” alisema Zitto.

Baada ya Membe kukubaliwa na Halmashauri Kuu kuwa mshauri wa chama hicho, Zitto alimwita jukwaani na kisha alipewa kiti.

Zitto alitoa pendekezo la Membe baada ya kuruhusiwa na mwendesha mkutano huo ambaye ni Maalim Seif. Membe alijiunga na chama hicho mwezi uliopita baada ya kufutiwa uanachama wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumzia hatua hiyo, Janeth Rite ambaye ni Naibu Katibu wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa chama hicho amesema, Membe ameteuliwa kutokana na uzoefu wake katika medani za siasa za Tanzania.

“Membe ni mbobezi katika medani za siasa Tanzania, hiyo ni miongoni mwa sababu iliyokisukuma chama na wajumbe wa Halmashauri Kuu kuridhia uteuzi huo,” amesema Janeth.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!