Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe akwama kupokelewa Lindi
Habari za Siasa

Membe akwama kupokelewa Lindi

Benard Membe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe pamoja na Maalim Seif
Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, amekwama kupokewa Lindi leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Sababu za kutopokewa na wananchi wa Lindi zimeelezwa na Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama hicho kwamba, fikra zao zimeelekezwa kwenye msiba wa Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu.

Mzee Mkapa amefariki dunia usiku wa kuamkia jana Ijumaa tarehe 24 Julai 2020, jijini Dar es Salaam.

Anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake Lupaso, Masasi Mkoa wa Mtwara tarehe 29 Julai 2020.

          Soma zaidi:-

Kuanzia kesho Jumapili hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020, Mwili wa Hayati Mpaka aliyeongoza Tanzania kati ya mwaka 1995 hadi 2005, utaagwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Zitto amesema, mapokezi ya Membe ambaye tayari amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania uras wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, yanasitishwa kwa muda.

“Tumeahirisha shughuli yetu ya kisiasa leo ya wananchi wa Lindi kumkaribisha Membe nyumbani ili kupisha shughuli za maombolezo ya Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa.”

“Tunaendelea kuwapa pole Watanzania na famiia ya Rais Mkapa kwa msiba mzito huu. Maisha ya Mkapa kiuongozi ni mafunzo,” ameandika Zitto kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Tayari baadhi ya viongozi waliokwenda Lindi kwenye shughuli za chama hicho ikiwa ni pamoja na maandalizi ya shughuli ya Membe, wamereja Dar es Salaam na kuhudhuria msibani kwa Mkapa, Masaki.

Miongoni mwa viongozi waliokuwa Lindi na Mtwara kwenye ziara ya chama hicho ni pamoja na Maalim Seif Sharif Hamad, mwenyekiti wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!