Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Membe akoleza moto urais Tanzania, atoa ombi Chadema
Habari za Siasa

Membe akoleza moto urais Tanzania, atoa ombi Chadema

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo
Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo amesema, kama vyama vya upinzani vitaweka ubinafsi pembeni na kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, milango ya kuingia Ikulu iko wazi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Pia, Mwanadiplomasia huyo mashuhuri, ameiomba kambi rasmi ya upinzani nchini humo kukubali kuungana ili kuiondoa Serikali iliyopo madarakani inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kambi ya upinzani inaundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Membe ametoa kauli hiyo leo Alhamisi tarehe 16 Julai 2020, baada ya kupokelewa rasmi na chama hicho katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar es Salaam.

Benard Membe (kushoto) akiwa na Zitto Kabwe pamoja na Maalim Seif

Miongoni mwa viongozi waliompokea Membe ni Maalim Seif Sharrif Hamad, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Ado Shaibu, Katibu Mkuu wa chama hicho.

Pia, makamu wenyeviti wa chama hicho, Juma Duni Haji (Zanzibar) na Doroth Semu wa Bara.

Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje, alifukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya chama hicho, kisha uamuzi huo kubarikiwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), tarehe 10 Julai 2020.

Membe alifukuzwa kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya CCM, pamoja na kuonywa mara kadhaa, pasina kubadilika.

Akizungumza ukumbini hapo, Membe amesema, “kwa vyama vyote vikubwa na vidogo kawaiga wenzetu wa Malawi (vyama vya upinzani viliungana na kushinda uchaguzi), tuache ubinafsi pembeni tuache tamaa zingine pembeni.”

Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa

“Tuungane pamoja katika ngazi ya taifa, tuende kifua mbele kuchukua uongozi wa nchi ambao barabara iko wazi nina imani na viongozi wa ACT-Wazalendo watalibeba hili,” amesema Membe.

Huku akishangiliwa, Membe amesema hakuna kipindi ambacho milango ya Ikulu iko wazi kama ilivyo sasa hivi.

“Upinzani kuwa na mgombea mmoja milango ya Ikulu iko wazi kuliko tangu tulipopata uhuru (mwaka Desemba 1961),” amesema Membe.

Mwanasiasa huyo ametoa wito kwa kambi ya upinzani nchini, kuungana kwa pamoja ili kuitoa Serikali iliyoko madarakani inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Naomba nitoe wito kwa kambi za upinzani, ni lazima tuungane ili tuweze kumtoa mtu yule Ikulu, ili tumpeleke nyumbani akapumzike ili turekebishe haya mambo kama tunavyopanga kwenye mkataba wetu na wananchi,” amesema Membe.

Membe amesema, “ni vizuri kambi ya upinzani, mimi nimeingia ACT lakini kambi ya upinzani ni kubwa tukitaka tuchewele tusiende Ikulu shauri yetu, tukitaka tusiungane tusiende Ikulu shauri yetu, tuungane.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!