January 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Membe aimwaga ACT-Wazalendo

Bernard Membe, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Spread the love

ALIYEKUWA mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ametangaza rasmi kujiuzulu uanachama na na nafasi ya mshauri mkuu wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea)

Amesema kwa sasa, atabakia kuwa mshauri kitaifa na kimataifa wa kushughulikia na kupigia debe masuala ya demokrasia kwa taifa lake.

Hatua ya kujiuzulu ameitangaza kijiji kwao Rondo- Chiponda Mkoani Lindi, nchini Tanzania leo Ijumaa tarehe 01 Januari 2021, wakati akizungumza na DW.

Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi zaidi juu ya sababu ya kuchukua maamuzi hayo.

Membe amesema,tayari ameandika barua ya kujiuzulu kwa kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kama utaratibu unavyotaka.

Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania katika utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Mrisho Kikwete amesema, kwa sasa ni mapema kubainisha mwelekeo wake unaofuata katika vyama vya siasa.

Membe alijiunga na ACT-Wazalendo Julai 2020 baada ya kufukuzwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kukiuka miongonzo na taratibu za chama hicho.

Uamuzi wa Membe ameuchukua ikiwa imepita miezi takribani miwili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambao yeye alikuwa mgombea urais.

Hata hivyo, mwanadiplomasia huyo, alitofautiana hadharani na viongozi wenzake akiwemo Zitto na Mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.

Zitto na Maalim Seif waitangaza hadharani kuwa ACT-Wazalendo ina muunga mkono mgombea urais wa Chadema, Tundu Lissu huku Membe akijitokeza hadharani kuwapinga na kuwasisitiza yeye ni mgombea halali.

error: Content is protected !!