BERNARD Kamilius Membe, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, amechukua fomu ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Membe ambaye ni Mshauri Mkuu wa chama hicho, amekabidhiwa fomu hizo leo Ijumaa tarehe 7 Agosti 2020, Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage
Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania katika utawala uliopita chini ya Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliongozana na mgombea mwenza, Profesa Omar Fakih Hamad.
Soma zaidi:-
-
Magufuli achukua fomu kuwania urais Tanzania
-
Watatu wachukua fomu za urais Tanzania
-
Membe ataja mtaji wa kumwingiza Ikulu, agusia katiba mpya
Pia, wamesindikizwa na viongozi wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad (mwenyekiti) na Katibu Mkuu wake, Ado Shaibu.
Juzi Jumatano, mkutano mkuu wa ACT-Wazalendo ulimteua Membe kugombea urais kwa kupata kura 410 sawa na asilimia 97 ya kura zote 420. Kura za wajumbe 10 zilimkataa.
Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo ulianza tarehe 5 utahitimishwa 25 Agosti 2020.
Kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020 na Uchaguzi Mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.
Leave a comment