Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdude: Nilitekwa, sihofii kifo
Habari za SiasaTangulizi

Mdude: Nilitekwa, sihofii kifo

Mdude Nyangari, mwanaharakati wa Chadema akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mkasa wake wa kutekwa na kuteswa
Spread the love

MWANAHARAKATI Mdude Nyagali, amehusisha kutekwa kwake na sababu za kisiasa huku akisisitiza kwamba, hatorudi nyuma. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

“Ninachojua ni kuwa, nilitekwa kwa sababu za kisiasa, siwezi kukimbia nchi kwa sababu ya hofu ya kifo,” amesema Mdude leo tarehe 20 Mei 2019 mbele ya waandishi wa habari.

Mdude amekutana na wanahabari kwenye Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Amesema, itikadi na ukosoaji wake kwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kupitia mitandao, ndio kulisababisha kutekwa na kuteswa.

Mwanahaharakati huyo alitekwa tarehe 4 Mei 2019 akiwa ofisini kwake Vwawa, Mbozi mkoani Songe na kupatikana baada ya siku tano, 9 Mei 2019) akiwa hoi katika eneo la Inyala, Mbeya vijijini.

Akizungumzia tukio la kutekwa kwake amesema, tarehe 4 Mei 2019 saa 12 jioni, alikamatwa na watu waliojitambusha kuwa polisi na kwamba, hata alipowaomba vitambulisho, waligoma kumwonesha.

“Nilipohojia juu ya kosa langu, wakaniambia kuwa wewe unatuhumiwa kumfachua rais pamoja na serikali yake kwenye mitandao,” amesema huku akibubujikwa machozi.

Hata hivyo amekiri kuwa, amekuwa akikososa serikali pale anapoona mambo hayaendi sawa, licha ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara kwa mara kwa tuhuma za kufanya uchochezi.

https://www.youtube.com/watch?v=2-pnPXNvM3I

Amesema, kutekwa kwake hakuna uhusiano na ujambazi kwa kuwa, hana pesa na anaishi chini ya Dola 100 za Marekani kwa mwezi, “jambazi anakuja kuchukua kwangu nini? Mimi kwa mwezi naishi chini ya dola mia (Sh 230,000).

“Ni jambazi gani anaweza kutumia magari mawili ambayo thamani yake ni zaidi ya milioni 300, aje kunipora mimi simu ya laki tatu la laptop ya laki saba?” amehoji.

Mwanaharakati huyo amesema, aliingizwa kwenye gari aina ya Landcruser kwa nguvu na baadaye kupigwa hadi kupoteza fahamu.

Amesema, mwaka 2016 alikamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Mbeya na kuwa, Mkuu wa Jeshi jijini humo alimtisha vinavyoashiria kuwa ndio matokeo yake.

Mdude amsema kuwa, wakati akipigwa na watekaji walikuwa wakimwambia “sisi sio wale wa kwanza, si ulishawahi kuzungumza na vyombo vya habari kwamba, ulikamatwa mara ya kwanza na ulipelekwa Osterbay, na ulichukuliwa Osterby sijui ukapelekwa kukojulikana na kuteswa ukiwa uchi, sasa sisi sio wale.

“Waambie hao wanaokutumia kwa sababu wewe hii sio akili yako, nyuma yako kuna watu, waambie hao Umoja wa Ulaya wanaokutuma waje wakuokoe, waambie hao Marekani waje wakuokoe, mwambie Mbowe aje akuokoe,” amesema Mdude.

Amesema, watu hao walimwambia kuwa, muda wanaomtesa Mbowe alikuwa amelala “Mbowe sasa hivi yupo wapi? amelala na mke wake. Sasa mpigie simu Lissu (Tundu Lissu) Ubelgiji aje akuokoe, mmekaa mmekosa uzalendo, serikali inafanya maendeleo halafu nyie mnapotosha umma.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!