Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdogo wa Lissu: Bunge limembagua Tundu
Habari za Siasa

Mdogo wa Lissu: Bunge limembagua Tundu

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki akiwa hospitali ya Nairobi
Spread the love

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linadaiwa kumbagua Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kilichodaiwa ni kutokana na Spika wa bunge hilo, Job Ndugai kutofika Hospitali aliyolazwa Mbunge huyo au kutuma hata kiongozi wa bunge pamoja na kutopewa uangalizi akiwa kama mbunge. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Vincent Mughwai, mdogo wa Tundu Lissu amesema kuwa kama mwanafamilia amesikitishwa sana na hatua hiyo ya bunge ambalo ndio ofisi ya kaka yake.

Vincent amesema amesema kitendo hicho kimeibua hisia tofauti kwa wanafamilia kwani viongozi wote waliofika wamekwenda kwa vyeo vingine lakini kimsingi ofisi ya bunge ambayo ilipaswa kuwa mstari wa mbele kufahamu kila kinachoendelea haitoi ushirikiano.

“Licha ya Bunge kutangaza kuchangia Sh. 43 milioni kwa matibabu ya Lissu, baada ya malipo ya pesa hizo tu kukamilika Lissu hakupewa stahili zake nyingine kama mbunge aliyekuwepo kwenye matibabu kama walivyofanyiwa wengine,” amesema.

Amesema kuwa Bunge na Familia vilikaa vikao ambavyo havikuzaa muafaka wa kumsaidia Lissu ambapo walitaka familia iandike barua ya kuomba kutibiwa kwa ndugu pamoja na kuandika barua hiyo, hakuna majibu yoyote yaliyotolewa wala matibabu.

“Bunge na Serikali zilitoa tamko la kuchangia matibabu ya Lissu iwe ndani au nje ya nchi pamoja na kwamba hiyo ni haki yake lakini hadi sasa hilo halikufanyika,” amesema Vincent.

Fuatilia Mazungumzo haya kupiti Youtube Channel yetu ya MwanaHALISI TV .. Pia usisahau kusubscribe channel yetu ili kupata taarifa mbalimbali kwa haraka zaidi.

1 Comment

  • Hivi Bunge lilipomkodia Tundu ndege imkimbize hospitali kwanini Chadema waliikataa na badala yake wakakodi ndege yao? Walikuwa na wasiwasi gani?
    Je sheria inamruhusu mbunge kujichagulia hospitali yake anayoipenda?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!