Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee na wenzake wafukuzwa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Mdee na wenzake wafukuzwa Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kimetangaza kuwafukuzwa uanachama wanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa tuhuma za usaliti. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetangazwa leo saa 5:11 usiku Ijumaa tarehe 27 Novemba 2020 na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa maazimio ya kikao cha kamati kuu.

Kikao cha kamati kuu kimefanyika kuanzia asubuhi leo katika Hoteli ya Bahati Beach jijini Dar es Salaam huku wajumbe wawili wa kikao hicho, Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa Chadema-bara na Ezekiel Wenje wakishiriki kwa njia ya mtandao.

Mdee na wenzake 18, walikuwa wakituhumiwa kujipeleka bungeni na kuapishwa tarehe 24 Novemba 2020 na Spika Job Ndugai wakijua chama hicho hakijatea majina ya wabunge wa viti maalum.

Wabunge wengine waliofukuzwa ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Ester Bulaya na Esther Matiko. Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje. Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), na Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha, Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa  na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao.Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Mbowe amesema, “Huwezi kupendekezwa na chama cha siasa, huwezi kupendekezwa na mtu yoyote kwani Tanzania hatuna mgombea binafsi. Sasa huwezi kupendekezwa na mtu yoyote yule,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema, Mchakato wote wa Katiba, Sheria na kanuni za Tanzania na vyama havikufuatwa kuwateua wabunge wengi 19 ,”Katibu mkuu hajawahi kujaza fomu namba 8(d). Sasa chama au kamati kuu haijateua au kupeleka majina, fomu hizo zipo ofisini mpaka sasa.”

“Wabunge wetu hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji.”

Amesema, Chadema kimeweka utaratibu kuwapata wagombea viti maalum udiwani, ubunge na uwakilishi ambao unaandaliwa na Baraza la wanawake (Bawacha) na kuwasilisha mapendekezo kamati kuu,”Lakini hakuna mapendekezo yaliyowasilishwa ila tunaona wameapishwa huko.”

Mbowe amesema, “Kamati kuu imewavua nyadhifa zao zote ndani ya chama na kuanzia sasa wasijihusishe kwa namna yoyote na masuala ya chama. Wako waliokuwa viongozi Bawacha na wengine Bavicha. Kamati tendaji za mabaraza hayo zikutane kujaza nafasi hizo.”

“Kiapo kilicholiwa Dodoma na mchakato mzima wa kuwapata, umegubikwa na uongo, kughushi na ulikuwa batili. Tumeagiza kurugenzi yetu kupinga huo uteuzi wa wabunge 19 na tutaupinga kwani chama hakijapelela majina,” amesema Mbowe

Mbowe amesema, “Wewe unakiasi chama, unaitwa mbele ya kamati kuu kuja kujieleza. Unakinajisi chama, unaitwa unaanza kutoa sababu eti upewe muda utafakari na barua zote 19 zinaonekana zimeandikwa na mtu mmoja.”

“Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 walioapa kule Dodoma. Milango iko wazi kuomba radhi kwa maadishi au kukata rufaa ndani ya siku 30 kwa baraza kuu kama wataona inafaa,” amesema Mbowe

Mbowe amesema, maazimio hayo yameungwa mkono kwa asilimia 100 na wajumbe wa kamati kuu

1 Comment

  • Lakini ilikuaje mpaka NEC na Supika wakurupuke na kuwaapisha kienyeji? Hawakudiriki hata kuzungumza na viongozi wa Chadema? Wanastahiki wachukuliwe hatua za kinidhamu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!