Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee: Gwajima?… tukutane jukwaani
Habari za Siasa

Mdee: Gwajima?… tukutane jukwaani

Spread the love

HALIMA Mdee, Mgombea Ubunge Kawe, Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema ‘Gwajima (Josephat Gwajima) kitu gani.’ Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, katika Jimbo la Kawe alilokuwa akiliongoza kwa miaka kumi mfululizo, mshindi atatokana na mkakati wake kwa wapiga kura.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 25 Agosti 2020, muda mfupi baada ya kurudisha fomu ya uteuzi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kugombea jimbo hilo na kukidhi masharti ya ujazaji wa fomu ya uteuzi.

Akimjibu mwandishi baada ya kuulizwa maandalizi yake ya kukabiliana na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima, mgombea wa CCM kwenye jimbo hilo amesema “Gwajima? Sina muda wa kujadili wagombea wenzangu, tukutane field (uwanjani). Kila mtu atashinda kwa mziki wake,” amesema Mdee.

Hata hivyo, amesema, zoezi la urudishaji fomu kwa upande wake halikuwa na changamoto yoyote kwani fomu yake imepokelewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!