CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelipa hukumu ya faini ya Sh. 100 milioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa ajili ya kuwakomboa viongozi wake wa kike. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea)
Hayo amesema Said Mohammed, Kaimu Mwenyekiti wa Chadema, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.
Mohammed amesema watakaolipiwa faini ni Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Esther Matiko, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Serengeti na Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini.
Amesema, Mdee amelipiwa faini ya Sh. 40 milioni, wakati Matiko akilipiwa faini ya Sh. 30 milioni, huku Bulaya akilipiwa faini ya Sh. 30 milioni.
Mohammed amesema kwa sasa mawakili wa chama hicho wanafuatilia kibali cha mahakama cha kuwatoa gerezani viongozi hao.
“Milioni 100 imetumika kwa maana tumepata kodi namba ya washtakiwa wetu, tumeenda kulipia. Tunasubiri mawakili kupata remove oda kwa ajili ya kumtoa Mdee gharama yake ni milioni 40 imelipwa. Matiko Milioni 30 imelipwa na Bulaya milioni 30 tumeshalipa,” amesema Mohammed na kuongeza:
“Tunategemea sana mawakili wetu wataweza kufanikisha leo hii na tutaungana nao ili kusaidiana nao kusuma ili lutoa viongozi waliobakia.”
Leave a comment