Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mch. Msigwa: Niligoma kutoka jela
Habari za SiasaTangulizi

Mch. Msigwa: Niligoma kutoka jela

Mchungaji Peter Msigwa
Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, aligoma kutoka jela. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari katika Makao Makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo tarehe 14 Machi 2020 amesema, sababu ya kuchukua uamuzi huo ni kutokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka kumtumia kwa maslahi ya kisiasa.

Msigwa alitoka jana tarehe 14 Machi 2020, baada ya kuelezwa kwamba Rais John Magufuli, amechangia Sh. 38,000,000 kuongezea kiwango cha Sh. 2,000,000 zilizochangwa na familia yake ili kumtoa jela.

Amesema, alimgomea Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezo wa CCM kujitokeza na kuoigwa picha wakati walipomfuata katika gereza la Segerea ili kumtoa.

“Wengine mmemuona Humphrey Polepole, natoka nje kuna kamera wakati juzi kina Halima (Halima Mdee-Kawe) wanatoka, kamera hazipo.

Nikasema, nirudishwe gerezani. Nilimwambie Polepole, mimi ni mtu ninayejitambua, siwezi kununuliwa kwa vipande 30 vya fedha, CCM kinajikanyaga,” amesema Mchungaji Msigwa.

Mchungaji Msigwa amesema, anao uhusiano wa kifamilia na Rais Magufuli huku akibainisha kwamba Polepole hana ukoo naye.

“Sio siri, mimi na Rais Magufuli tuna mahusiano ya kifamilia. Ninachosema Polepole sio mwana familia yetu, mambo ya familia yanamuhusu nini?

“Mahusinao yangu na Rais Magufuli yanazungumzwa kifamilia sio hadharani. Ninaomba tusihame kwenye mjadala wa msingi, tukazungumza ya kifamilia,” amesema na kuongeza:

“Nakwenda bungeni, nitavaa nguo za wafungwa kuonesha nchi hii iko kifungoni. Sisi wabunge hatujaiba, tunatetea demokrasia. Tumefika hapa waliomuuwa Akwilina wako barabarani.

“Waliozuia vitambulisho wako barabarani. Wale walioleta shida hii wanatembea katika taifa lililokua la kidhalimu. Sisi tunaotaka haki tumepelekwa gerezani. Tunapambania na utawala wa haki”

John Heche, Tarime Vijijini amesema, alijiandaa kufungwa, na kwamba hatorudi nyuma kutompigia magoti yeyote kutokana na dhuluma wanayofanyiwa.

“Kwa jinsi ambavyo tumenyimwa haki mahakamani, nilijiandaa kufungwa na si faini. Nataka kusema, sitapigia mtu magoti kwa kitendo cha kufungwa au kuuawa. Yale ninayoamini nitapigania mpaka tone langu la damu la mwisho,” amesema Heche aliyepewa namba 302 ya ufungwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!