Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mch. Msigwa amchongea Mkuu wa Mkoa kwa Lukuvi
Habari Mchanganyiko

Mch. Msigwa amchongea Mkuu wa Mkoa kwa Lukuvi

Spread the love

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amemshitaki Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi kwamba amekuwa akiwaruhusu wananchi kujenga ovyo bila kufuata matumizi bora ya mipango miji. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka bungeni Jijini Dodoma…(endelea).

Mbunge huyo akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumatano tarehe 30 Januari 2019 amesema kuwa, licha ya kuwa Iringa ni mkoa wa kwanza kuzindua Master Plane na Waziri Lukuvi kusisitiza wananchi kufuata mpango huo, lakini kwa mkuu wa mkoa huyo amekuwa akikiuka kauli ya waziri na kuwataka wananchi kuendeleza ujenzi holela.

Katika swali lake alitaka serikali Mchungaji Msigwa alitaka serikali itoe kauli ni kauli ipi iweze kusikilizwa na wananchi kati ya Waziri Lukuvi au Mkuu wa Wilaya wa Wilaya ya Iringa.

Awali katika swalila msingi la Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema) alitaka kujua ni lini kampuni binafsi zinazofanya ya upimaji zitatoa hati za ardhi au leseni za makazi kwa wananchi.

Aidha alitaka kujua ni vikwaza gani vinakabili zoezi la upimaji na serikali inachukua hatua gani kuviondoa ili kuzisaidia kampuni hizo kumaliza kazi zao kwa haraka pia alitaka kujua ni lini serikali itakamilisha mpango kabambe mpya wa Jiji la Dar es Salaam ili uwe dira katika upimaji,na urasimishaji.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angella Mabulla alisema kuwa ni yema ujenzi utafuata taratibu za mpango miji kwani hiyo ndiyo taratibu ambayo inatakiwa kufuatwa.

Alisema kuwa licha ya kuwa ofisi ya wizara haijapokea malalamiko yoyote lakini siyo sahihi kuhamasisha watu kujenga kiholela  na wakati huo Mabulla alisema kuwa serikali inatambua kuwa mkoa wa Iringa ndiyo wakwanza waliozindua mpango wa ujenzi wa matumizi bora ya ramani(Master Plane).

Aidha alisema kuwa kwa sasa hakuna vikwazo vyovyote vinalolikabili zoezi la urasimishaji ardhi nchini zaidi ya changamoto ya mwitikio mdogo wa wananchi katika maeneo mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!