Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mch. Gwajima: Hii ni vita, nainua makombora
Habari Mchanganyiko

Mch. Gwajima: Hii ni vita, nainua makombora

Spread the love

ASKOFU Josephat Gwajima, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini amesema, kusambazwa kwa video ya ngono inayodaiwa kuwa yake, ni vita kwake na sasa anainua makombora. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Amesema, alijua kuwa vita imeisha (hakutaja vita yake na nani) na kwamba, silaza na makombora vimewekwa chini lakini sasa, makombora yameinuliwa tena.

Akizungumza na waandishi wa habari leo terehe 8 Mei 2019, Askofu Gwajima amehusisha usambazaji wa video hiyo na masuala ya kisiasa huku akisisitiza kwamba, aliyefanya hivyo anamjua.

Video hiyo imeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii jana tarehe 7 Mei 2019, ambapo inamuonesha mtu anayedaiwa kuwa Askofu Gwajima, akifanya ngono na mwanamke.

Mbele ya wanahabari Askofu Gwajima amesema, video hiyo imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kumziba mdomo ili asizungumze katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Amedai kuwa, tabia yake ya kuzungumza katika vipindi vya uchaguzi ndio sababu ya kuzuka kwa tukio hilo na kwamba, halitamrudisha nyuma, ataendelea na desturi yake hiyo.

“Nilijua sasa yameisha, vita vinavyoisha si unaweka silaha chini? Aliyekuwa na jembe visu, panga na makomboti, anarudisha makombora yake ghalani. Lakini ukiona mtu amebeba makombora yake, anaanza kurusha na wewe unabeba yako,” Askofu Gwajima na kuongeza;

“Na mwaka wa uchaguzi umekaribia nipo, hapa anyong’onyei mtu. Hata kama ungesambaza, ungepanga watu pembeni ukasema hawa ni wa Gwajima, swali la kipumbavu linavutia jibu la kipambavu na matendo ya kipumbavu unajibu kipumbavu, mjibu mpumbavu pamoja na upumbavu wake asijejiona mwelevu kwa wengine.”

Aidha, Askofu Gwajima amesema, mtu aliyesambaza video hiyo analengo la kumchafua kwa familia, kanisa na waumini wake.

“Kwa miaka yote, mmeniona pakitoka maovu huwa nakemea awe mfalme, rais au mbunge, na nitaendelea na hiyo kazi. Kwa nini ni mimi, asitafute mtu mwingine?  Kwa nini anakwenda mahala ambapo atasagwasagwa, anajua ataishia kupoteza?

“Kwenye ulimwengu wa leo, kuna mahala ambapo natakiwa niseme hiki, lazima niseme tena kwa usahihi bila kumung’unya maneno, na hii ndio sababu ya watu kuleta matukio ili nikose sauti, nataka niwaambie ndio nimeanza, safari hii itakuwa kali kuliko zamani.”

Akifafanua kuhusu video hiyo, Askofu Gwajima amesema, ni ya kutengenezwa kwani picha zilizotumika ni zile alizopiga akiwa na familia yake, huku akisisitiza kwamba, video hiyo si halisi kutokana na kuwa, baadhi ya viungo vinavyoonekana ndani yake si vya kwake.

“Haiwezekani mwili uwe wa mwingine na kichwa cha mwingine, picha ya kwanza ameweka picha ya familia nikiwa kifua wazi, (akionesha picha ambayo yuko na mke wake). Ndio picha ya kwanza inaonesha ninaibuka,” amesema Askofu Gwajima.

Askofu Gwajima amesema, amechukua hatua kadhaa kuhusu tukio hilo, ikiwemo kuitaarifu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) pamoja na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwachukulia hatua watu waliohusika kusambaza video hiyo na kulichafua jina na hadhi yake.

“Nimechukua hatua za awali, nimechukua RB nimeiambia TCRA wamtafute huyo aliyeisambaza impate. Nitajua sheria inafanya kazi, siwezi kuchafuliwa mimi sheria isifanye kazi, nichafuliwe mimi asipatikane?

“Kila silaha itakayofanyika juu yangu, mimi haitafanikiwa, nitakuwa na nguvu kubwa kuliko nilizo nazo leo, nitasema kuliko nilivyosema mwaka jana, niko tayari kusema zaidi ya nilivyosema uchaguzi uliopita,”

Mke wa Askofu Gwajima, Grace Gwajima amesema, tuhuma hizo si za kweli kwani anamfahamu na kumuamini mume wake kwamba, hawezi kufanya jambo kama hilo.

Grace amesema, hakuna mtu atakayefanikiwa kubadili msimamo wake wa kumuamini mumewe na kwmaba atasimama naye daima.

“Waovu hukimbia pasipo kufuatiliwa na mtu, lakini wenye haki ni majasiri kama simba, mimi ni jasiri kama simba, ukweli nina ufahamu, mume wangu ninamfahamu na ninamuamini na ukweli huo hakuna mtu anayeweza kuubadilisha.

“Niko pamoja na yeye,  nitasimama pamoja na yeye na Mungu akiwa upande wetu hakuna atakayetutenganisha,” amesema Grace.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!