Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yampa uongozi wa LAAC aliyefukuzwa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

CCM yampa uongozi wa LAAC aliyefukuzwa Chadema

Spread the love

ALIYEKUWA katibu mkuu wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), nchini Tanzania, Grace Tendega, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC). Anaripoti Danson Kaijade, Dodoma…(endelea).

Tendega ambaye amefukuzwa uanachama wa chama hicho, kufuatia kupatikana na tuhuma za usaliti, alichaguliwa kushika nafasi hiyo jana Jumatatu mjini Dodoma.

Nafasi ya makamu mwenyekiti wa LAAC, imechukuliwa na Suleiman Zedi (CCM).

Wabunge hao wawili, walikuwa wagombea pekee kwenye nafasi hizo na kila mmoja amepata kura 22. Kamati hiyo, ina jumla ya wajumbe 25.

Tendega, pamoja na wabunge wengine 18 wa Viti Maalum ambao walikuwa wanachama wa Chadema, walifutuwa uanachama wa chama hicho na Kamati Kuu (CC), iliyokutana Novemba mwaka jana.

Wote kwa pamoja, walituhumiwa kwa usaliti ndani ya Chadema, kujipeleka bungeni kuapishwa bila idhini ya chama hicho, udanganyifu, ugombanishi, kuchochea migogoro na kushirikiana na wanaokitakia mabaya chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

          Soma zaidi:-

 

Uteuzi wa Tendega unathibitisha madai ya baadhi ya wadadidi wa kisiasa, kwamba kitendo cha waliokuwa wanachama hao wa Chadema kujipeleka bungeni kinyemela, kililenga kunufaisha CCM na serikali yake.

Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Kamati mbili za LAAC na Hesabu za Serikali (PAC), zinapaswa kuongozwa na upinzani.

Hata hivyo, kutokana na kutokufikiwa kwa akidi, Bunge hili, halitokuwa na Kambi Rasmi ya upinzani bungeni, maarufu kama “kambi ya waliowachache.”

Wote 19 kwa pamoja, wamekata rufaa kwa Baraza Kuu la Chadema kupinga kufukuzwa unachama, hoja ambayo ni ngumu kukubaliwa.

Mbali na Grace kufukuzwa, wengi  ni wale waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,  Halima Mdee, Ester Bulaya na Esther Matiko. Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje.

Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa  na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao.Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

1 Comment

  • Yaani hawa watakuwa wanawakilisha chama gani? Ni kambi ya upinzani au ya chama tawala? Kwani kila mbunge lazima awe na chama kilichomteua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!