Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Lwakatare, kula matapishi yake?
Habari za Siasa

Mbunge Lwakatare, kula matapishi yake?

Wilfred Lwakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini
Spread the love

WILFRED Muganyizi Lwakatare, mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Bukoba Mjini, mkoani Kagera, aliyetangaza kustaafu mbio za ubunge, yuko mbioni kubadilisha maamuzi yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na Lwakatare zinasema, uamuzi wa mbunge huyo kurejea tena katika ulingo wa kisiasa, unatokana na kile kinachoitwa na wafuasi wake, “kuombwa na viongozi wake wakuu katika Chama cha Wananchi (CUF), wakiongozwa na Prof. Ibrahim Lipumba.”

Lwakatere amenukuliwa mara kadhaa akisema, amepanga kustaafu ubunge, mara baada ya kumaliza muhura wake huu wa sasa wa ubunge.

Bunge la Jamhuri, limepangwa kufungwa rasmi na Rais John Magufuli, tarehe 19 Juni mwaka huu.

Alisema, mara atakapostaafu ubunge, atajishughulisha na shughuli za kilimo nyumbani kwake mjini Bukoba, na ataweza kusaidia vyama vya upinzani ushauri wa jinsi ya kushinda uchaguzi.

“Nakuambia hivi, kuna kila dalili kuwa mheshimiwa Lwakatare atagombea tena ubunge katika jimbo la Bukoba Mjini,” ameeleza mmoja wa viongozi wajuu wa CUF na kuongeza, “hii inatokana na chama na viongozi wake, kumuomba afanye hivyo.”

Amesema, “CUF wanaamini Lwakatare bado ana nguvu na uwezo wa kushinda jimbo la Bukoba Mjini. Ndio maana wanamng’ang’aniza kugombea tena. Naye anaonekana kuwa yuko tayari kubadili maamuzi yake kwa maslahi ya chama chake.”

Kupatika kwa taarifa hizi, kumekuja wiki moja yangu Lwakatere apokelewe kwa mbwembwe na uongozi wakuu wa CUF, makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kujiunga na Chadema mwaka 2019, Lwakatare alikuwa mwanachama wa CUF. Ndani ya chama hicho, ameshika nafasi mbalimbali, ikiwamo Naibu Katibu Mkuu (Bara); mbunge wa Bukoba Mjini (2000 hadi 2005) na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.

Akihutubia makumi ya wanachama wa chama hicho, katika mapokezi hayo, Lwakatare alisema, CUF kimempa heshima kubwa; anaweza kufikiria mara mbili uamuzi wake wa kustaafu ubunge.

Lwakatare ambaye alikuwa mbunge na mwanachama wa Chadema, hadi Mei mwaka huu, alipovuliwa uwanachama, ameibua gumzo kubwa kufuatia matamshi yake, kwamba katika uchaguzi mkuu ujao, amejipa “kazi ya kupambana na Chadema.”

Lwakatare alifukuzwa Chadema na wenzake watatu, tarehe 9 na 10 Mei mwaka huu, kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Wengine waliovuliwa uanachama na Lwakatare, ni pamoja na Anthony Komu (Moshi Vijijini); David Silinde (Momba) na Joseph Selasini (Rombo).

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika aliwaambia waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, kwamba wabunge hao wamefukuzwa uanachama na kwa kosa la kukaidi agizo la kutaka wasiingie bungeni kwa siku 14 ili kujikinga na Corona (Covid 19).

Alisema, mbali na kukaidi maelekezo ya Kamati Kuu (CC) ya Chadema, Lwakatare, Komu, Selasini na Silinde, wamefukuzwa uanachama wa chama hicho, kwa madai ya kutoa kauli za kejeli dhidi ya viongozi wao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Bukoba, uamuzi wa Lwakatere kurejea kwenye ulingo wa kisiasa, unatarajiwa kutokea Ijumaa wiki hii, wakati atakapohutubia mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa Uhuru, mjini Bukoba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!