Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Komu: Yakinishinda Chadema, nitaondoka
Habari za Siasa

Mbunge Komu: Yakinishinda Chadema, nitaondoka

Anthony Komu, Mbunge wa Moshi Vijijini
Spread the love
MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Moshi Vijijini, Anthony Komu “amesema, ikiwa Chadema itamshinda, atajiunga na chama kingine cha upinzani.” Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

“Sijawahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wala sitarajii kujiunga na chama hicho,” ameeleza Komu na kusisitiza, “kama mambo yanayoendelea ndani ya Chadema yatanishinda, nitajiunga na chama kingine, lakini siyo CCM.”

Komu alitoa kauli hiyo leo tarehe 19 Februari 2020, katika mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) ya chama cha NCCR- Mageuzi, jijini Dar es Salaam. Amehudhuria mkutano huo kama mgeni mwalikwa.

Amesema, “…kwa hiyo ndugu zangu, naomba hili niliseme wazi, kwamba mimi kama mambo yaliyopo Chadema yatanishinda, siendi Lumumba (ofisi za CCM); nitaenda chama kingine cha upinzani.

“Na kushindwa Chadema, ni jambo la kawaida kabisa. Kwa  sababu, Chadema siyo mama yetu; hivyi vyama ni vyombo tu vya kutufikisha tunakokwenda.”

Komu ambaye alikuwa mmoja wa waasisi wa mageuzi nchini na mwanzilishi wa NCCR- aliondoka chama hicho, mwaka 2002, baada ya kutofautiana na baadhi ya viongozi wenzake, kufuatia maamuzi yao ya kuwawekea pingamizi wagombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Visiani.

Mwanasiasa huyo na wenzake kadhaa, wakiwamo baadhi ya wabunge wa Chadema, wanadaiwa kuwapo kwenye mgogoro mkubwa na baadhi ya viongozi wenzao kwenye chama hicho, akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jambo ambalo linawafanya wao kufikiria kuondoka ndani ya Chadema.

Taarifa zinasema, tayari baadhi ya viongozi hao, wamekata shauri la kujiunga na NCCR- Mageuzi. Haijaweza kufahamika mara moja, ikiwa Komu naye atarejea katika chama chake hicho, ingawa kuna uwezekano mkubwa wa hilo kufanyika.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Komu alisema, hatua ya viongozi wa NCCR-Mageuzi, kumualika kushiriki mkutano huo, imempa faraja, hasa katika kipindi hiki anachosakamwa na wenzake ndani ya Chadema.

Hata hivyo, Komu hakuwataja kwa majina anaodai, “wanamsakama ndani ya Chadema.”

Lakini Komu alisema, “nimshukuru mwenyekiti na uongozi mnzima wa NCCR –Mageuzi, viongozi wa Halamshauri Kuu ya Taifa kwa kunialika kwenye kikao ili niweze kutoa uzoefu wangu katika safari hii ya kujenga mageuzi nchini kwetu. Hii ni heshima ya peke kwangu na imenipa faraja hasa wakati huu ambao ninasemwa semwa sana. Ninyi mmenithamini sana. Mungu awabariki.”

Akizungumzia kuhusu wanachama wa Chadema waliorejea CCM, mwanzishi huyo wa NCCR- Mageuzi aliyekuwa na kadi Na. 6 amesema, “nawatakia safari njema”

Amesema, “Mbatia akitaka kwenda aende aone kama  hiki chama kitakufa. Augustine Mrema, alikuwa mwenyekiti wa chama, akaondoka chama kikawepo; Prof. Ibrahim Lipumba aliondoka wakati wa uchaguzi, lakini Chama cha Wananchi (CUF), kiliimarika zaidi. Vyama ni vya wanachama; siyo mali ya mtu mmoja.”

Komu amesema viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa kufanya shughuli za ujenzi wa vyama vyao badala ya kunyoosheana vidole.

“Tuacheni kunyosheana vidole, tufanye kazi kwa kila mmoja kwa kutimiza wajibu wako.  Jenga chama chako. Leo unaisikia watu wanatoka povu wanamlaumu Lowassa (Edward Lowassa), wanamlaumu Sumaye (Fredirick Sumaye), eti wamerudi CCM.

“Mimi nasema, naheshimu maamuzi yao. Lowassa na Sumaye, ni watu wa kwanza kwa madaraka yao, kuthubutu kuingia upinzani. Lowassa ametuletea mambo mengi. Ameondoka, lakini hataondoka nayo yote,” amesisitiza.

Komu anafahamika kutoka na historia yake ya kuendesha na kusimamia vuguvugu la mageuzi nchini katika miaka ya 1990, wakati huo, akiwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika kitabu kilichopewa jina la “Vyama Vingi Vyaja,” Komu anatajwa kuwa mmoja wa wawezeshaji wa semina ya mageuzi Kuelekea Mfumo wa Vyama Vingi vya Siasa nchini, iliyofanyika katika kkumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Kwenye kongamano hilo, Komu alieleza umuhimu wa wanafunzi na vijana, kupigania demokrasia ya vyama vingi.

Wengine waliotoa madai, ni Mabere Marando ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kongamano hilo; Christopher Kansanga Tumbo, Prince Bagenda, Omar Aweis Dadi na Ndimara Tegambwage.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!