Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge Joseph Musukuma na wenzake wapandishwa kizimbani
Habari Mchanganyiko

Mbunge Joseph Musukuma na wenzake wapandishwa kizimbani

Spread the love

MBUNGE wa Geita Joseph Musukuma leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama Hakimu Mkazi Geita, kujibu tuhuma zake zinazomkabili, baada ya kushikiliwa na polsi tangu jumapili ya wiki iliyopita, anaandika Mwandishi wetu.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kumpeleka Mahakamani mbunge huyo, ambaye anatuhumiwa kuhusika na kuratibu vurugu katika mgodi wa GGM mkoani humo.

“Wamepelekwa Mahakamani asubuhi hii”, amesikika Kamanda Mwabulambo akisema.

Mbunge huyo pamoja na baadhi ya wadiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola milioni 12.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!