Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema atoboa siri ya wizi wa Sh. 2.4 trilioni  
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Chadema atoboa siri ya wizi wa Sh. 2.4 trilioni  

Spread the love

MBUNGE wa Viti Maalum mkoani Mara, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Catherine Ruge, “ameivua nguo serikali.” Amesema, kiasi cha Sh. 2.4 bilioni, kitakuwa ama kimeibwa au hakijulikani matumizi yake. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jana Ijumaa, tarehe 1 Februari 2019, Ruge alisema, kuna ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba serikali imeshindwa kuithibitishia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), jinsi ilivyotumia mabilioni hayo ya shilingi.

Alisema, pamoja na kufanyika uhakiki kwenye hoja ya matumizi ya Sh. 1.5, kumeibuka hoja nyingine mpya. Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, amethibitisha kuwapo kwa wizi makubwa ya fedha za umma yanayofanywa na serikalini kinyume na taratibu.

Amesema, mbali na kiasi cha Sh. 1.5 trilioni, kutoonekana matumizi yake, kiasi kingine cha Sh. 2.4 trilioni, kimetumika bila kufuata utaratibu; na au fedha hizo zimeibwa.

Akiongea kwa kujiamini, Ruge alisema, “..mhe naibu spika, naomba niweke rekodi clear (sahihi), sio kazi ya CAG kusema kama kuna wizi. Yeye kazi yake, ni kufanya ukaguzi na kutambua mapungufu yaliyopo na kuiacha kazi hiyo ya utambuzi kwa mamlaka zinazohusika.”

Anaongeza, “katika hili, CAG amefanya kazi yake. CAG ametimiza wajibu wake. Ni jukumu la mamlaka nyingine, kufanya uchunguzi ili kupata kueleza kama fedha hizo zimeibwa au zimetumika kihalali.”

Ruge ambaye aliingia bungeni, tarehe 4 Mei 2017, kufuatia kifo cha Dk. Elly Marco Macha, alidai kuwa ndani ya Hazina ya taifa, kumekosekana nyaraka za kuthibitisha matumizi ya Sh. 2.4 trilioni, “jambo ambali ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kamati ya PAC, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, alithibitisha kuwapo kwa wizi mkubwa serikalini na kwamba kiasi cha Sh. 2.4 trilioni, hazikuonekana matumizi yake.

Kwa sasa, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali, ni Prof. Mussa Assad. Siku 10 zilizopita, Prof. Assad huyu huyu alitiwa misukosuko mikubwa na Spika Ndugai kwa madai kuwa amelidhalilisha Bunge.

Spika Ndugai alitoa amri kwa Prof. Assad kufika kwa hiari yake mbele ya Bunge – vinginevyo angekamatwa na kufikishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka – akiwa na pingu mikononi. Prof. Assad alitii agizo hilo.

Ruge aliyehudumu kwenye kamati ya PAC kwa takribani mwaka mmoja na nusu, ameliambia Bunge kuwa mkaguzi huyo wa fedha za umma (CAG), amenukuliwa na kamati hiyo akisema, “kuna tofauti ya Sh. 1.5 trilioni, kwenye mfuko mkuu wa fedha za Serikali (HAZINA) ambazo hazikukaguliwa wakati anafanya ukaguzi wake kwa hesabu zilizoishia mwaka wa fedha wa 2016/2017.”

Alisema, analishukuru Bunge la Jamhuri kwa hatua yake ya kumuagiza CAG kufanya ukaguzi maalum kwenye mfuko mkuu wa serikali (Hazina). Akaishukuru pia Kamati ya PAC kwa uamuzi wake wa kuleta hoja hiyo bungeni na kwamba kwa kupitia ukaguzi huo, kumeibuliwa hoja kadhaa ambazo serikali imekosa kuzijibu.

“Kwenye hii ripoti maalum ya ukaguzi, kuna suala la ya over draft ya Sh. 290.7 bilioni. Katika hili, Hazina wanasema, hii ilikuwa overdraft na kwamba fedha hizi zilikwenda kwenye miradi ya maendeleo na hazikupita kwenye mfuko mkuu wa Hazina. Lakini CAG hakupata vielelezo vyovyote vinavyothibitisha maelezo hayo,” ameeleza Ruge.

Ruge anasema, “CAG alienda mbali zaidi. Aliamua kuomba conformation letter (barua ya uthibitisho) kutoka Benki Kuu ya taifa (BoT), ili kujiridhisha salio la Sh. 290.7 bilioni. Akatoa barua ya uthibitisho kutoka BoT ambayo inaeleza kutokuwapo hata shilingi kwenye akauti hiyo kuu ya serikali.

Alisema, “akaunti ya mfuko mkuu wa serikali, kulikuwa na zero balance (sirufi), wakati Hazina inafunga mahesabu yake Juni mwaka 2017. Ripoti ya ukaguzi na hesabu hiyo ninayo hapa.”

“Kuna pia tarifa za ukaguzi wa BoT za Juni 2017, zinazoonyesha kuwapo kwa balance (salio) ya overdraft ya central bank (BoT), inayozungumzia hiyo Sh. 1.5 trilioni. Lakini mheshimiwa spika, nina hansard hapa (taarifa ya kumbukumbu sahihi ya Bunge) ya tarehe 20 Aprili 2018 ukurasa 22 hadi 25, ambapo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji,aliposimama bungeni kutoa majibu ya serikali kuhusu tofauti ya 1.5 trilioni.

Akimnukuu Dk. Kijaji alisema, over draft ilikuwa Sh. 79.1 bilioni, sasa hapa tuna figa nne za kutoka kwenye serikali moja. Tuamini  ipi na tuiache ipi,” alihoji.

Alihoji, “tuamini ile ya BoT ya Sh. 1.5 trilioni ambayo barua yake ya uhamishi ilisoma “zero balance, au melezo ya naibu waziri inayozungumzia Sh. 79.1 ama taarifa ya hesabu ya BoT ya Sh. 1.5 trilioni? Yaani kwa kifupi, naona serikali inapoteana.”

Hata hivyo, mbunge wa Buda Vijijini (CCM), Boniface Mwita Getere, alitoa taarifa kuwa anachokizungumza Ruge hakimo kwenye ripoti ya Kamati ya Bunge iliyowasilisha ripoti hiyo bungeni.

Aidha, Getere alisema, Hazina walifafanua kuwa utoaji huo wa fedha za umma unaoidi ya mapato, ni kwa mujibu wa kifungu cha 34 cha sheria ya BoT ya mwaka 2006.

Akijibu hoja hiyo, Ruge alisema, alikuwa mjumbe wa Kamati na hivyo anafahamu kila kitu kuhusu kilichoripotiwa na CAG mbele ya kamati yake ya PAC.

Alitaja hoja nyingine kuwa inahusu Sh. 976.69 bilioni. Fedha hizo zilifanyiwa mgawo kwenye vote mbalimbali kutoka Hazina kwenda kwenye voti 20 na kwamba fedha hizo hazikupitishwa na Bunge.

Alisema, “fedha hizo zilizokwenda kwenye voti 20 (ofisi ya rais, usalama wa taifa), hazikukaguliwa kutokana na CAG kuzuiwa kisheria, kukagua voti hiyo. Hata mgawanyo wake haukupata Baraka za BoT. Kwa hiyo serikali inakitumia kifungu hiki, kama kichaka chake.

Alisema, “hizi fedha hazikupata approve ya CAG (baraka). Hoja hii haipo kwenye taarifa ya kamati, lakini pia mpaka leo hii, Hazina haijatoa majibu.”

Ruge alikumbushia kauli aliyoitoa Dk. Kijaji, tarehe 20 Aprili 2018, bungeni mjini Dodoma, kwamba kulikuwa na nyaraka  za Sh. 687 bilioni ambazo zilisababisha tofauti ya 1.5 trilioni na kwamba hilo lilitokana na Hazina kuanza kutumia mfumo wa Ipsaz, lakini taarifa ya CAG inaonyesha tofauti.

Alisema, “hoja nyingine ni ya hati fungani.  Hazina walikuja na vielelezo ambavyo vilikuwa kwenye excel na CAG amesema, ‘hizi taarifa haziaminiki.’”

Akimnukuu CAG mbele ya kamati ya PAC, Ruge alisema, “kinachoshangaza inakuwje Hazina inatumia mfumo wa Excel kuweka hesabu zake ambao unaweza  kubadilishwa kwa kuongezwa kitu? Hivi tuko makini kweli?

“Hazina ambako tunaamini kunalindwa fedha za walipa kodi wanyonge, ndiko tunakoshuhudia matatizo haya na udhaifu huu wa mfumo. Udhaifu huu mkubwa wa Hazina yetu usipofanyiwa kazi, taifa hili litaingia kwenye matatizo makubwa.”

Alisema, hata hati fungani zilionekana kuiva, CAG alisema, vielelezo vyake vilileletwa kwenye mfumo wa Excel na ukiangalia hiyo taarifa ukijumlisha na hati fungani hizo, “figa ya Sh. 659 bilioni haipatikani. Inakuja Sh. 853 bilioni na hivyo kuonekana tofauti ya kilichosemwa na serikali na kile kilichoelezwa na CAG.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!