Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema amvaa Spika Ndugai, ampa kazi ngumu
Habari za Siasa

Mbunge Chadema amvaa Spika Ndugai, ampa kazi ngumu

Spread the love

NAIBU waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Viti Maalumu, Jesca Kishoa (Chadema) amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndigai kumuita mwanasheria mkuu wa serikali kutokana na mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza maelekezo ya CAG ya kuwepo kwa ufisadi wa kutisha katika kampuni ya SONGAS. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo alisema kuwa anasikitishwa na serikali ya awamu ya tano ambayo imekuwa ikijipambanua kuwa inapambana na ufisadi katika miradi mbalimbali ya serikali lakini imeshindwa kuchukua hatua katika mradi wa kampuni ya SONGAS kutokana na kuingia mkataba wa kifisadi.

Kishoa alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kutokana na kauli ya Spika Ndugai kumwita Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa madai kuwa amelidhalilisha bunge kwa kuliita dhaifu wakati akihojiwa na kituo kimoja wapo cha utangazaji cha Umoja wa mataifa.

Kishoa alisema kuwa Kampuni ya SONGAS ni kampuni iliyoingia mkataba wa kifisadi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mara kadhaa amekuwa akipiga kelele kama mbunge na kama waziri kivuli wa Nishati na madini lakini serikali imekuwa ikikaa kimya huku ikijinadi kuwa ni serikali ya kupambana na ufisadi.

“Nimewaita kuzungumza nanyi ili muweze kufikisha ujumbe kwa wananchi wa Tanzania kuhusu ufisadi mkubwa unaoendelea katika kampuni ya SONGAS, ni kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ili ingia mkataba na serikali ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 20 kuanzia mwaka 2004 hadi 2024.

“Gharama za mradi wa SONGAS  ilikuwa ni Euro 392 milioni, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mradi huo imetoa Euro 285.7 milioni sawa na asilimia 73 ya mradi mzima, huku kampuni ya SONGAS ikitoa Euro 106.3 milioni sawa na asilimia 27 ya mradi.

“Ufisadi katika mradi wa SONGAS upo katika maeneo matatu ambayo ni mfumo mzima wa uwekezaji na umliki wa mradi, makataba wa Capacity Charges,” alisema Kishoa.

Aidha alieleza kuwa serikali ya Tanzania inamiliki mradi kwa silimia 46 pekee yake na SONGAS inamiliki mradi kwa asilimia 54, na kama serikali iliwekeza asilimia 73 ya mradi mzima wa SONGAS iliwekeza asilimia 27 ya mradi mzima, inakuwaje SONGAS imiliki mradi kwa kiwango kikubwa wakati iliwekeza mtaji mdogo jambo ambalo linaonesha wazi kuwa ni wizi wa fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Alisema kuwa kila mwezi Serikali ya Tanzania kupitia TANESCO imekuwa ikilipa SONGAS Capacity Charge ya dola 5 milioni ambapo Capacity Charge ni fedha za fidia anayopewa mwekezaji kufidia gharama aliyotumia kuwekeza, ambapo lengo kubwa la serikali kumiliki mitambo ya SONGAS baada ya mkataba kwisha.

Alieleza kuwa kila dola 5 milioni ya capacity charge inayotolewa kila mwezi na serikali kuipa SONGAS kuna dola 3.6 milioni zilitakiwa kwenda serikalini, lakini serikali inaipatia SONGAS fedha zote za fidia wakati serikali ndiyo iliyowekeza kwa kiasi kikubwa kuliko SONGAS.

Kishoa alisema kuwa tangu kuanza kwa mradi wa SONGAS mwaka 2004 hadi 2018 serikali imeisha poteza zaidi ya Sh. 1.3 trilioni na ifahamike kuwa mkataba huo unakoma mwaka 2024 na kama serikali serikali itapuuza itapoteza kiasi cha trilion mbili kwa kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.

“Kilichotufikisha katika hasara hii ya kifisadi ni udhahifu wa Bunge kwa sababu ufisadi huu ulishawahi kuzungumzwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini chini ya Mwenyekiti William Shelukindo mwaka 2005 kwenye taarifa yake Bungeni ukurasa wa 8, Ripoti ya CAG Ludovick Uttoh ya mwaka 2009 ukurasa wa 135, Ripoti ya CAG, Profesa Mussa Assad ukurasa wa 131 ya mwaka 2018 na mimi mwenyewe Naibu Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nilizungumzia suala hili zaidi ya mara tatu Bungeni lakini hakuna hatua zinazochuliwa na Bunge.

“Napenda kutoa rai yangu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Spika wa Bunge, waandishi wa habari na watanzania wote kwa ujumla, Rai yangu kwa Rais Dk. John Magufuli hasira zake alizotuonyesha katika ufisadi wa  IPTL sasa ni muda mwafaka kuzionesha kwa SONGAS.

“Rai yangu kwa spika Job Ndugai mwanasheria mkuu wa Serikali (AG) aitwe mbele ya Kamati ya Maadili kwa kulidanganya na kulipuuza Bunge mbele ya kiti chake ndani ya Bunge na siyo nje ya nchi kwa kusema kuwa atalishughulikia suala la SONGAS ndani ya miezi miwili tangu Mei 5 mwaka 2018 lakini hadi leo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Bunge  lililopita  nilihoji na hakunijibu,” alieleza Kishoa.

Katika hatua nyingine amewaeleza watanzania kuwa pamoja na yeye kuwa mume wake ambaye alikuwa mwana mageuzi na kuondoka na kujiunga na CCM na kupewa kazi na serikali lakini bado lakini yeye (Kishoa) anaendelea kupambana na kutetea maslahi ya wananchi kwa faida ya watanzania kwa ujumla.

Alisema kuwa ikumbukwe kuwa mume wake ambaye ni David Kafulila anaendelea kumuunga mkono (Kishoa) kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi ndani ya serikali bila kujali kuwa yeye ni pinzani na Kafulila yupo serikalini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!