Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema amkabili JPM mkutanoni
Habari za Siasa

Mbunge Chadema amkabili JPM mkutanoni

Spread the love

PASCHAL Haonga, Mbunge wa Mbozi (Chadema), amemweleza Rais John Magufuli namna matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo zinavyofanya kazi katika kutekeleza shughuli za kijamii. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Leo tarehe 4 Oktoba 2019, akiwa jimboni humo, Haonga amemueleza Rais Magufuli, kwamba fedha za mfuko wa jimbo huzitumia katika shughuli za kijamii, na husoma taarifa ya matumizi hayo kwa wananchi.

Haonga ametoa ufafanuzi huo baada ya Rais Magufuli kumhoji kwenye mkutano na wananchi, sababu za yeye (Haonga) kushindwa kutatua changamoto ya wananchi ya kulipishwa michango ya shule wakati ana fedha za mfuko wa jimbo, kama wanavyofanya wenzake.

“Kwa nini hujaizuia na wewe ni mbunge wa jimbo hili?  Angalau kwenye mchango utoe zile hela unazolipwa na serikali za jimbo, ukafidia kwenye mchango ndivyo wanavyofanya wenzako. Zako zinachangia wapi?” alimhoji Rais Magufuli.

Sakata hilo liliibuka baada ya baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo kulalamika, kwamba wanalipishwa michango mingi na Halmashauri ya Mbozi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya shule, ambapo hutozwa hadi Sh. 25,000 kila mzazi.

“Mheshimiwa rais, fedha za mfuko wa Jimbo la Mbozi zimeletwa katika kata hii ya Maenge na vijiji vyote 6. Hapa kuna shule inajengwa, tumepeleka fedha pamoja na katika ujenzi wa zahanati na kadhalika. Tunaomba tusaidie kwenye michango ipungue ili wananchi hawa wapate pesa za kununua mbolea,” amemjibu Haonga.

Baada ya malalamiko hayo, Rais Magufuli alimuagiza Erick Ambakisye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi kutoa ufafanuzi wa michango hiyo.

Akitoa ufafanuzi wa michango hiyo, Ambakisye amesema ni kweli utaratibu huo upo na ulipitishwa na Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo, na kuwa kila mwananchi hutozwa Sh. 10,000 kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ya shule.

“Kweli tumekuwa na utaratibu wa miaka yote kwa kila mwananchi kutoa mchango wa 10,000 kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ya shule zetu.

“Katika wilaya yetu ya Mbozi, ndio walioweka utaratibu na ni ahadi zao za kampeni, hatuwezi kuwaingilia,” ameeleza Ambakisye.

Ambakisye amesema, utaratibu huo umewekwa kutokana na wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa, ambapo wanafunzi 167 wanakaa katika darasa moja.

“Tuna kata 29 katika Wilaya ya Mbozi. Hii ndio kata pekee ambayo miundombinu ya shule si mizuri, chumba kimoja cha darasa wanakaa wanafunzi 167.

“Katika utaratibu ambao mbunge ameueleza, ni sehemu ya utaratibu ambao Baraza la Madiwani limeupitisha na yeye akiwemo. Tukakubaliana kwa pamoja mpaka hivi leo tumejenga vyumba 1,510,” amesema Ambakisye.

Kufuatia changamoto hiyo, Rais Magufuli ametoa fedha kiasi cha Sh. 5 milioni, kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na vyumba vya madarasa vya Shule ya Sekondari Lumbila iliyoko wilayani Mbozi, Songwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!