Mbunge Chadema aliyekamatwa, atoka ‘sero’

JESHI la Polisi wilayani Tarime limewaachia kwa dhamana, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) na Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Sitta Tuma. Anaripoti Regina Kelvin…(endelea).

Matiko na Tuma walikamatwa jana tarehe 8 Agosti, 2018 na Jeshi la Polisi wakiwa kwenye mkutano wa kumnadi mgombea udiwani Chadema Kata ya Turwa.

Polisi waliuzuia mkutano huo kwa sababu ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Tarime kuzuia mikutano ya chama hicho.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema Matiko na Tuma wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena polisi hapo kesho.

Vile vile, Polisi imewaachia kwa dhamana wanachama wa Chadema kumi na nane waliokamatwa jana katika mkutano huo.

JESHI la Polisi wilayani Tarime limewaachia kwa dhamana, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko (Chadema) na Mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, Sitta Tuma. Anaripoti Regina Kelvin…(endelea). Matiko na Tuma walikamatwa jana tarehe 8 Agosti, 2018 na Jeshi la Polisi wakiwa kwenye mkutano wa kumnadi mgombea udiwani Chadema Kata ya Turwa. Polisi waliuzuia mkutano huo kwa sababu ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Tarime kuzuia mikutano ya chama hicho. Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema Matiko na Tuma wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuripoti tena polisi hapo kesho. https://twitter.com/zittokabwe/status/1027506916241678337 Vile vile, Polisi imewaachia…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram