Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge Chadema akerwa maagizo ya JPM kupuuzwa
Habari za Siasa

Mbunge Chadema akerwa maagizo ya JPM kupuuzwa

Wakati wa Kata ya Mkundi mkoani Morogoro
Spread the love

TABIA ya baadhi ya watendaji wa serikali kupuuza maagizo ya Rais John Magufuli kumemkera Mbunge wa Viti Maalum Chadema. Anaripoti Tibason Kaijage, Dodoma…(endelea).

Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) ameitaka serikali itoe kauli na kulieleza Bunge kwanini baadhi ya watendaji ndani ya serikali wamekuwa wakikiuka maagizo yanayotolewa na Rais Pombe.

Devotha ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Februari 2019 bungeni alipouliza swali la nyongeza. Amesema kuwa, wakati Rais Magufuli alipokuwa Morogoro kwenye ziara, aliagiza wananchi wa CCT Mkundi katika Manispaa ya Morogoro wasibughudhiwe.

“Lakini hivi sasa maofisa wa maliasili wanaendelea kuwabughudhi wananchi wale. Ni kwanini maofisa hao wanaendelea kukiuka agizo la Rais?” amehoji.

Awali katika swali la msingi la Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi (CCM) amehoji serikali ina mpango gani wa kuwalipa fidia wananchi wa Igwata ili waweze kununua meneo mengine ya kufanya shughuli za kilimo?

Aidha mbunge huyo ameleta hoja hiyo leo bungeni huku akifafanua kuwa, mipaka ya mradi wa mafunzo ya masitu wa Kijiji cha Igwata, Kata ya Nyabubinza, Maswa imepanuliwa na kuchukua baadhi ya mashamba ya wanakijiji hivyo kusababisha wananchi kukosa maeneo ya kulima.

Akijbu swali la nyongeza lililoulizwa na Deviotha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amesema, maofisa wa Maliasili kwa maana ya TFS wanafanya kazi kwa kusimamia sheria hasa kwa mipaka iliyopo katika maeneo husika.

Na kwamba, kama kuna maagizo yaliyotolewa na rais, ataenda kufuatilia na kuona ni kwa namna gani maofisa hao wanakiuka maelekezo hayo.

Pamoja na mambo mengine naibu waziri huyo amesema, Msitu wa Hifadhi wa Igwata unafadhiliwa kisheria kwa tangazo la serikali Na.324 la mwaka 1954.

“Msitu huo una eneo la ukubwa wa hekta 132.851 ambapo hekta 85.19ziko wilaya ya Kwimba na hekta 47.678 ziko wilaya ya Maswa,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!