Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge CCM aibana Serikali ubovu wa mashine za EFD’s
Habari za Siasa

Mbunge CCM aibana Serikali ubovu wa mashine za EFD’s

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kutoa taarifa ya uhakika juu ya sakata la kutofanyakazi kwa Mashine za Kieletroniki (EFD’s) huku ikidaiwa kuwa kitendo cha mashine hizo kutofanya kazi na serikali kukaa kimya ni hujuma kwa uchumi wa nchi. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Sakata hilo lilibuliwa jana Bungeni baada ya Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndasa, kuitaka serikali kutoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo alilolifananisha na hujuma kwa uchumi wa nchi.

Ndasa amesema kuwa tangu Juni 11 mwaka huu hadi sasa, mashine hizo hazifanyi kazi na mnunuzi yeyote wa bidhaaa hawezi kupatiwa risiti za kieletroniki, hivyo mapato ya kodi stahiki ya serikali yanapotea.

Mbunge huyo ameomba maelezo hayo ya serikali leo baada ya kuomba mwngozo kwa Mwenyekii wa Bunge, Mussa Zungu, wakati ambao Bunge likiwa linaendelea na mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Amesema kuwa tangu tarehe aliyoitaja mtu yoyote akienda kununua kitu hawezi kupewa risiti za kieletroniki na kueleza kuwa kutokana na hali hiyo ni hakika kuwa mapato mengi ya serikali yatapotea.

“Ningependa kujua sasa, kwa sababu wiki ya kwanza, ya pili na ya tatu mashine hizi hazifanyi kazi, je, serikali inasemaje kuhusu tatizo hili ambalo ni janga la kitaifa?,” amehoji.

Ndasa amesema tatizo hilo linawezekana likawa ni hujuma kutoka kwa watu wasioitakia mema nchi.

Mara baada ya Ndasa kuomba ufafanuzi, huo Zungu alimtaka Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashantu Kijaji, kutoa kauli ya serikali Bungeni.

Akitoa kauli kuhusu sakata hilo, Dk. Ashantu ameeleza na kukiri kuwa ni kweli tatizo hilo lipo tangu Mei 11 mwaka huu, lakini lilishughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi ndani ya wiki moja hata hivyo lilijirudia tena.

“Sasa hivi taasisi yetu ya E-Governament (Wakala wa Serikali Mtandao) kwa kushirikiana na kitengo cha ICT cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaendelea kulishughulikia kwa nguvu zote ili hali ijurudie kama kawaida,” amesema Dk. Ashantu.

Amesema serikali inafahamu changamoto za tatizo hilo na ndio maana wataalam bado wanaendelea kulishughulikia na matumaini yaliyopo litapatiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!