Mbunge wa Jimbo la Mtera na mtia nia wa jimbo hilo, Livingstone Lusinde

Mbunge CCM ahojiwa kwa ‘kugawa’ rushwa

Spread the love

TAASISI ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemuhoji Lingstone Lusinde, aliyekuwa Mbunge wa Mtera (CCM) kwa tuhuma za kugwa rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kwa mujibu wa Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma, Lusinde alifikishwa katika ofisi za taasisi hiyo zilizoko wilayani Chamwino, Jumatano tarehe 8 Julai 2020.

Kibwengo amesema, Takukuru ilimuita na kumuhoji Lusinde, baada ya kupata taarifa ya kwamba, wajumbe wa vikao vya uteuzi wa wagombea wa CCM nyumbani kwake, kwa minajili ya kuwapa fedha kama kishawishi ili wampitishe kugombea katika uchaguzi huo.

Kibwengo amesema, baada ya mwanasiasa huyo kuhojiwa, aliachiwa na kuwamba uchunguzi juu ya sakata hilo unaendelea.

“Tulipata taarifa ya kwamba anakusanya wapigakura nyumbani kwake awapatie fedha kama kishawishi. Jana tulimhoji ofisini kwetu Chamwino, na kisha tuliamuachia. Lakini uchunguzi unaendelea,” amesema Kibwengo.

Lusinde alikuwa mbunge wa Mtera kwa vipindi viwili mfululizo, kuanzia mwaka 2010-2015 hadi 2015-2020.

TAASISI ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemuhoji Lingstone Lusinde, aliyekuwa Mbunge wa Mtera (CCM) kwa tuhuma za kugwa rushwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea). Kwa mujibu wa Sosthenes Kibwengo, Mkuu wa Takukuru mkoani Dodoma, Lusinde alifikishwa katika ofisi za taasisi hiyo zilizoko wilayani Chamwino, Jumatano tarehe 8 Julai 2020. Kibwengo amesema, Takukuru ilimuita na kumuhoji Lusinde, baada ya kupata taarifa ya kwamba, wajumbe wa vikao vya uteuzi wa wagombea wa CCM nyumbani kwake, kwa minajili ya kuwapa fedha kama kishawishi ili wampitishe kugombea katika uchaguzi huo. Kibwengo amesema, baada ya mwanasiasa huyo kuhojiwa, aliachiwa na kuwamba uchunguzi juu ya sakata…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!