January 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Bwege atangaza kutimkia ACT-Wazalendo

Suleiman Bungara 'Bwege', aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini (CUF)

Spread the love

SELEMAN Bungara maarufu ‘Bwege,’ Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) amesema, kuanzia kesho Jumanne Juni 16 2020 baada ya Bunge kuhitimishwa, atajiunga na chama cha ACT-Wazalendo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Bwege ameweka wazi dhamira hiyo leo Jumatatu tarehe 15 Juni 2020, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema, amefanya uamuzi huo kutokana na kuona Chama cha Wananchi (CUF) hakina, muafaka  kwenye siasa za mabailiko.

Bwege amesema, haiendi ACT-Wazalendo kwa kumfuata Maalim Seif Sharif Hamad amekwenda kwa kuwa chama hicho ni kipya, “kambare mkunje angali mbichi” ACT tunaweza kuikunja.”

Maalim Seif aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, alitimkia ACT-Wazalendo baadhi ya viongozi na wanachama baada ya kutokea kwa mgogoro wa uongozi.

error: Content is protected !!