Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ataka wabakaji wahasiwe, AG amtuliza
Habari za Siasa

Mbunge ataka wabakaji wahasiwe, AG amtuliza

Spread the love

ZAINABU Katimba, Mbunge wa Viti Maalimu (CCM), ameishauri serikali kuweka adhabu kali kwa wabakaji ikiwemo kuhasiwa. Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Akizungumza bungeni leo tarehe 4 Februari 2020, Zainabu amesema, masharti ya kuthibitisha ubakaji yamekuwa magumu hasa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18, na kwamba ni vema utaratibu huo ukaangaliwa vizuri.

“Kigezo au masharti ya kuthibitisha kosa la ubakaji ni mpaka yule aliyebakwa athibitishe kama kulikuwa na kuingiliwa (yaani penetration), na mazingira hayo ni magumu sana katika utaratibu wa kawaida na hasa kwa watoto.

“Je, serikali haioni kwamba, kufanyike marekebisho ya sheria ili kuongeza adhabu kwa wale watakaothibitika kwamba wamefanya kosa la ubakaji…,kwa mfano serikali haioni kwenye kosa la ubakaji, mbakaji apewe adhabu ya kuhasiwa?” ameuliza Zainabu.

Akijibu hoja ya Zaibau, Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amempongeza kwa kusimamia haki za watoto na wanawake.

Hata hivyo amesema, katika kutoa ushaidi, wameondoa vigezo vilivyokuwepo ikiwa ni pamoja na kutoruhusu mtoto aliyefanyiwa ukatili kutoa ushaudi mahakamani.

“Tumeondoa baadhi ya vigezo ambavyo vilikuwepo hasa watoto kuweza kutoa ushaidi wenyewe, na kuiwachia mahakama uamuzi wa busara,” amesema.

Amesema, adhabu zilizopo mpaka sasa ni kali ikiwemo miaka 30. Na kwamba, kama itabidi kuongeza adhabu kama ambavyo mbunge alivyoshauri, bunge likae pamoja.

“Kama itabidi kuongeza adhabu hizo, baada ya marekebisho na mapitio ya sheria hizi, ninashauri Bunge likae na tushuriane tuweze kuzungumzia suala hili, linahitaji uamuzi wa kisheria,” amesema.

Prof. Aderlardus Kilangi, Mwansheria Mkuu wa Serikali (AG) amesema, sheria iliondoa baadhi ya mambo yaliyoelezwa kuwa ni viashiria vya ubakaji kwa aliyebakwa na kwamba, ilikuwa kama udhalilishaji.

“Lakini mwisho wa siku, haya yote lazima yafuate misingi ya jinai kwamba lazima kuthibitisha pasipo kuacha shaka, ili kuwa anayetuhumiwa asije akatuhumiwa ama akampewa adhabu isivyo sahihi.

“Na katika hili suala la kuongeza adhabu, tayari sheria ile imeiongeza adhabu na imekuwa kali sana hadi miaka 30, sasa hili pendekezo la kuhasiwa lina tatizo moja, litatupelekea kuvunja Katiba,” amesema.

Amefafanua kwamba ibara ya 13(6), inaeleza kuwa ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu zinazomdhalilisha.

“Kwa hiyo, tukichukua pendekezo la kuhasiwa, linatupeleka tena katika upande mwingine ambapo tunaweza kuvunja Katiba,” amesema.

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya amesema, sheria peke yake hata ziwe kali kwa kiwango chochote, haziwezi kumaliza tatizo la ubakaji na ulawiti kwa watoto.

Amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutimiza wajibu wa malezi kwa watoto “mtoto anabakwa kwa miezi mitatu bila mzazi kujua, unajiuliza hivi huyu mtoto ana wazazi? Narudisha mzigo kwa wazazi na walezi, tutimize wajibu wetu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!