Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ashangaa Ranchi ya NARCO kubadilishwa matumizi
Habari za Siasa

Mbunge ashangaa Ranchi ya NARCO kubadilishwa matumizi

Sophia Mwakagenda
Spread the love

SERIKALI imetakiwa ieleze, kwanini Ranchi ya NARCO Mbarali iliyoanzishwa kwa ajili ya mifugo, imeacha matumizi yake na sasa eneo hilo linatumika kwa kilimo? Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Swali hilo limeulizwa na Sophia Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) leo tarehe 14 Aprili 2020, jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali majibu.

Wizara ya Mifugo ikijibu swali hilo imeeleza, Ranchi ya Usangu iliyopo wilayani Mbarali ni miongoni mwa ranchi ambazo serikali ilielekeza zigawanywe katika vitalu na kukodishwa kwa wawekezaji, ili kuendeleza ufugaji wa kisasa na kibiashara kwa mikataba maalum.

Wizara imesema, katika mpango huo, Ranchi hii iligawanywa katika vitalu 16 vyenye ukubwa wa kati ya hekta 2,448.90 hadi 3,158.88 na kukodishwa kwa wawekezaji wazawa. Kwa sasa Ranchi hiyo ina jumla ya ng’ombe 9,885, mbuzi/kondoo 6,192, punda 56 na farasi wawili (2).

“NARCO imekwishafanya tathmini na kubaini jumla ya wawekezaji katika vitalu vitano ambao wamekiuka masharti ya uwekezaji kwa kutumia mashamba hayo kwa shughuli za kilimo.

“Hivyo NARCO imechukua hatua za kisheria, ikiwemo kutoa notisi za kuonesha nia ya kuvunja mikataba na kuwaondoa wawekezaji hao na maeneo yao yatakodishwa kwa wafugaji wengine wenye nia ya kuwekeza kwa mujibu wa sheria,” wizara imeeleza na kuongez:

“Ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, NARCO kwa sasa inaendelea na zoezi la kuweka mipaka inayoonekana katika Ranchi zake zote ikiwemo Ranchi ya Usangu.”

Wizara imeeleza kuwa, imeanzisha mpango wa kuwakodisha wafugaji maeneo kwa muda mfupi kwa utaratibu wa mikataba maalum.

“Katika mwaka 2019/2020, jumla ya vitalu 107 vimekodishwa kwa wafugaji katika Ranchi zake zote. Aidha kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbarali, NARCO imeanza zoezi la kuwabaini wafugaji walio tayari kuwekeza katika maeneo ambayo wataondolewa wawekezaji waliokiuka masharti ya mkataba,” imeeleza wizara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!