MBUNGE Alfred Yekatom maarufu kama Rambo, aliyekamatwa na vyombo vya dola baada ya kufyatua risasi bungeni nchini Afrika ya Kati (CAR) amefikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Rambo amekuwa mtu wa kwanza kutoka CAR kupelekwa ICC akikabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo kuhusika kwenye mauaji, kuteswa watu, kuwashambulia raia na kuwaingiza watoto kwenye shughuli za kijeshi.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya uhalifu huo mwaka 2013 hadi 2014 kwa kuongoza kundi la wapiganaji la waumini wa kikikristo Anti-Balaka, baada ya kundi la waislamu la Seleka kuipindua serikali mwaka huo.
Rambo mnamo mwaka 2016 alichaguliwa kuwa mbunge licha ya kuwkewa vikwazo na Umoja wa Mataifa (UN).
Leave a comment