June 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe, wenzake kujitetea siku tano mfululizo

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kuanza kusikiliza utetezi wa viongozi tisa  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), siku tano mfululizo kuanzia tarehe 7 mpaka 11 Oktoba, 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Utetezi huo ulitarajiwa kuanza tarehe 17 Septemba, 2019, lakini ulishindikana kutokana na baadhi ya washtakiwa Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini walikuwa udhuru baada ya wamepata msiba wa ndugu zao wa karibu, ndipo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alilazimika kuharisha utetezi huo.

Viongozi wanaoshtakiwa kwenye kesi hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, Vincent Mashinji, Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika, Naibu Katibu Bara, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Zanzibar.

Wengine ni Mchungaji Msigwa, Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, Heche, Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Wakili wa upande wa utetezi ambao watakuwa na kazi ya kuwaongoza Mbowe na wenzake katika utetezi huo wanaongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Jeremiah Mtobesya, Hekima Mwasipu, John Mallya, Frederick Kihwelo na Dickson Matata.

Upande wa Serikali, mawakili wao wanaongozwa na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu, Dk. Zainab Mango, Wakili wa Serikali Mkuu, Wankyo Simon, Wakili wa Serikali Mwandamizi, na Jackline Nyantori, Wakili wa Serikali.

Katika utetezi huo kunatarajiwa kuwepo mashahidi wa upande wa utetezi ambao wana majeraha ya risasi ambaye waliyapata siku ya tukio hilo.

Naye Hakimu Simba amesisitiza kuwa anataka kuimaliza kesi hiyo kwa kuwa ina muda mrefu hivyo ameutaka upande wa utetezi kuzingatia ratiba za mahakama.

Kwenye shauri hilo namba 112 la mwaka 2018, Mbowe na mwenzake wanashtakiwa kufanya maandamano yaliyokinyume cha sheria, kutoa maneno ya uchochezi na kusanyiko haramu lililosababisha kuuawa kwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwelin.

error: Content is protected !!