Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, wenzake kiguu na njia polisi
Habari za Siasa

Mbowe, wenzake kiguu na njia polisi

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe wameripoti Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Wengine ni, Godbless Lema, mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob wameripoti leo Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020.

Viongozi hao wanatuhumiwa kuratibu, kuhamasisha na kuwezesha maandamano ya amani nchi nzima yenye lengo la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

Mbowe na wenzake waliripoti kituoni hapo kukidhi masharti ya dhamana waliyopewa Jumanne tarehe 3 Novemba 2020.

Baada ya kuripoti kituoni hapo, Mbowe amesema wametakiwa kuripoti tena kituoni hapo Jumatatu tarehe 9 Novemba 2020.

“Tulitakiwa turipoti leo kwa RCO msaidizi Mkoa wa Kinondoni, tumefanya hivyo mimi, Zitto, Lema, Jacob na Halima Mdee. Tumetakiwa turipoti tena Jumatatu, hatujui sababu za kwenda na kurudi lakini tumepokea maelekezo,” amesema Mbowe.

Halima Mdee, aliyekuwa ubunge wa Kawe kwa tiketi ya Chadema

Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Edward Bukombe amesema, wanasiasa hao wameripoti kituoni hapo leo kwa ajili ya kuendelea na taratibu nyingine kuhusu tuhuma zinazo wakabili.

“Wameripoti tena kwa tuhuma za kuandaa maandamano yasiyo koma. Baada ya juzi kupewa dhamana leo wameripoti na taratibu zingine zinaendelea kwa mujibu wa sheria,” amesema Bukombe.

Mbowe na Zitto tarehe 31 Oktoba 2020 waliitisha maandamano ya amani yasiyo na kikomo kupinga matokeo Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, wakitaka urudiwe chini ya Tume Huru ya Uchaguzi.

Matokeo hayo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), yalikipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo aliyekuwa Mgombea wake wa Urais wa Tanzania, Dk. John Magufuli alishinda kwa asilimia 84 huku kikitwaa majimbo zaidi ya 255 kati ya 264.

Aliyekuwa mpinzani wa karibu wa Dk. Magufuli katika uchaguzi huo kupitia Chadema, Tundu Lissu alishinda kwa asilimia 13.

Dk. Magufuli ameapishwa leo Alhamisi Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kuongoza tena Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!