Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Matiko waitwa Mahakama ya Rufaa
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Matiko waitwa Mahakama ya Rufaa

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakiwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam
Spread the love

KESI ya kupinga kurejeshewa dhamana iliyofunguliwa na serikali dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasim na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Mwekahazina wa Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA), Esther Matiko, itasikilizwa Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Februari mwaka huu. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Serikali iliwasilisha Mahakama ya Rufaa, maombi ya kuwazuia Mbowe na Matiko kurejeshewa dhamana zao. Ni baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kutupilia mbali mapingamizi ya serikali yaliyotaka mahakama hiyo kutosikiliza shauri lililofunguliwa na Mbowe na Matiko.

Kwa mujibu wa vyanzo via taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa na ambazo zimethibitishwa na Prof. Abdallah Safari, ambaye anaongoza jopo la mawakili katika kesi hiyo, ni kwamba “Mbowe na Matiko, watafika mbele ya majaji wa mahakama ya rufaa, Jumatatu ya tarehe 18 Februari.”

Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro na Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni, alifutiwa dhamana na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.

Katika uamuzi wake, mahakama ilisema, maelezo yaliyotolewa na Mbowe, mdhamini wake na wakili wake, yalilenga kuidanganya mahakama.

Naye Matiko ambaye pia ni mbunge wa Tarime Mjini, alifutiwa dhamana na mahakama baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa mara mobile mfululizo kwa maelezo kuwa alikuwa nje ya nchi kwa shughuli za Bunge.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!