FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewaomba viongozi wa dini kuliombea taifa, ili liwe salama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).
Mbowe ametoa wito huo kwenye ibada maalumu ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mzee Elias Mwingira, Baba wa Nabii na Mtume wa Kanisa la Huduma ya Efatha, Josephat Mwingira, leo tarehe 22 Februari 2020, Kibaha mkoani Pwani.
Kiongozi huyo wa Chadema amewaomba viongozi wa dini zote nchini, kuungana kwa pamoja katika kumuomba Mungu, ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani.
“Ombi langu maalum kwako Nabii na Mtume Josephat Mwingira, wewe na viongozi wengine kutoka dini zote, mkaungane kuliombea taifa katika mwaka huu wa uchaguzi,” ameomba Mbowe.
Wakati huo huo, Mbowe amewaomba viongozi wa dini kuwaombea viongozi wa vyama siasa ili Mungu awape unyenyekevu.
“Pia mkatuombee sisi Viongozi wa kisiasa tuache viburi, tuvae unyenyekevu, tukawe na tume huru ya uchaguzi katika uchaguzi ujao, haki ikatamalaki” amesema Mbowe.
Great content! Super high-quality! Keep it up! 🙂