May 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbowe awaachia kibarua Watanzania 28 Oktoba

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amewaomba Watanzania kuutumia Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020, kuamua mustakabali mwema wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Mbowe ametoa ombi hilo jana Jumatatu tarehe 19 Oktoba 2020, wakati akimuombea kura Mgombea Urais wa Tanzania wa Chadema, Tundu Lissu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Moshi Mjini mkoa wa Kilimanjaro.

Mwenyekiti huyo wa Chadema ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Hai, aliwaomba Watanzania, watafakari nchi yao ilipotoka, iliko na inakoelekea ili kuutumia uchaguzi huo kurekebisha makosa yaliyojitokeza.

“Watanzania wote, nahitaji kila mwananchi aungane na mamilioni ya Watanzania wengine kuitafakari nchi hii imetoka wapi, iko wapi na inaenda wapi.  Tumeona matendo ya kikatili sana, tunataka wananchi wawe huru,” alisema  Mbowe

“Kwa sasa, wanaumzwa wafanyabiashara, Tunawaambia wana siku nane, baada ya siku nane masuala kama haya lazima Watanzania  tuyamalize kwa kumpigia kura za kishindo Tundu Lissu, wagombea udiwani na ubungo,” alisema

error: Content is protected !!