Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe ataja sababu ya kukacha kugombea urais
Habari za Siasa

Mbowe ataja sababu ya kukacha kugombea urais

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, ameacha kugombea urais ili ajenge chama hicho. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Mbowe alieleza nia yake ya kutaka kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama hicho ili agombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, hata hivyo hakuchukua.

Kwenye chama hicho, wanachama 11 walieleza kuwa na ya kuchukua fomu na kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho Mbowe akiwemo. Hata hivyo, ni wanachama saba tu ndio waliojitokeza kuchukua fomu, kujaza na kurejesha.

          Soma zaidi:-

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema leo tarehe 3 Agosti 2020, jijini Dar es Salaam amesema amekacha mbio za kugombea urais wa Tanzania ili akijenge chama hicho.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Mbowe amesema, tamaa zake haziwezi kuwa na thamani, ikilinganishwa na thamani ya Chadema, hivyo ameipa dhamani Chadema kuliko mbio za urais.

“Nilifatwa nikaambiwa mwenyekiti gombea urais, hofu ikaibuka mwenyekiti anagombea, makamu anagombea, nikasoma kwenye mitandao lakini mimi binafsi kama Mbowe hiki chama kwangu ni kama mtoto, haiwezekani tamaa zangu binafsi zikawa za maana kuliko uhai wa chama chetu,” amesema Mbowe.

Mbowe amesema, hatoiacha safari ya kuijenga Chadema kwa sababu ya maslahi yake binafsi. “Tumeumua sana kuijenga Chadema, hatutaiacha safari hiyo kwa sababau ya masilahi binafsi,” amesema Mbowe.

Wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakisubiri kuanza kwa kikao hicho

Akizungumzia mkutano huo uliolenga kutafuta jina moja kati ya majina ya watu waliotia nia kugombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema, Mbowe amewataka wajumbe kuchagua mgombea anayefaa na kuepuka mipasuko.

“Nguvu yetu ni umoja wetu, tutoke hapa wote tuna nyuso za furaha, tumpate mgombea katika mazingira ya kuujenga umoja wetu na sio mpasuko kati yetu,” amesema M bowe.

Wakati huohuo Mbowe amewasihi wajumbe wa baraza hilo kutowabagua WanaChadema waliowahi kuwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Tunahitaji kuonyesha upendo ndani ya chama chetu kuimarisha Tanzania kujenga umoja wetu, hatuhitaji kufanya makosa ya CCM kutubagua na sisi tukafanya ubaguzi dhidi ya wanachama wenzetu sababu walikuwa CCM, tunahitaji umoja wa kitaifa, tunahitaji mtu mmoja,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!