Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe anena, kurudi kwa Tundu Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe anena, kurudi kwa Tundu Lissu

Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki
Spread the love

TAARIFA za ujio wa Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki zimekolezwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Bupe Mwakiteleko…(endelea).

Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema, amezungumza na Lissu kuhusu kurejea kwake nchini akithibirita tarehe rasmi kuwa 7 Septemba 2019.

Taarifa za kurejea kwake zimekuwa zikikoleza mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), likieleza kuanza kuandaa maandalizi ya kumpokea.

Lissu ambaye alikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) ameeleza kuwa, safari ya kurejea Dar es Salaam, Tanzania itaanza baada ya kukutana na madaktari wake tarehe 20 Agosti 2019, kwa ajili kuangalia afya yake na kwamba, baada ya hapo atakuwa akikutana nao kila baada ya mwaka.

Hata hivyo Mbowe amesema, tarehe 7 Septemba ni muhimu kwa watu wanaopigania demokrasia nchini kwa kuwa, ilikuwa siku ya shambulio la demokrasia na kurejea siku hiyo ni historia.

Lissu alishambuliwa tarehe 9 Septemba 2017, akiwa nyumbani kwake Dodoma muda mfupi baada ya kutoka kuhudhuria vikao vya Bunge mchana wa siku hiyo.

Baada ya kushambuliwa, Lissu alipelekwa katika Hospitali ya Rufani ya Dodoma kwa matibabu ya awali, siku hiyo hiyo usiku alihamishiwa Nairobi, Kenya na baadaye alipelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Lissu katika siku za karibuni alizua mijadala hasa baada ya kuanza ziara zake katika nchi za Ulaya na Marekani, Bunge nalo liliingia kwenye mjadala huo likimtaka arejee nyumbani kwa kuwa, hakukuwa na taarifa ya ugonjwa wake kwenye Ofisi ya Spika

Tarehe 19 Januari 2019 Lissu alihojiwa katika kipindi cha Dira ya Dunia, Idhaa ya Kiswahili ya BBC. Tarehe 21 Januari 2019, Lissu alihojiwa kwenye kipindi cha HardTalk kupitia BBC.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!